gillana
Member
- Jul 7, 2018
- 81
- 83
Habarini wadau;
Katika kijiji cha Majimaji wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma kimevamiwa na tembo wengi wanao kadiriwa kuwa arobaini ambao kwa sasa wamekuwa sehemu wakazi wa kijiji hicho kwa takribani miezi mitano mfulululizo bila kutolewa kurudi katika hifadhi yao ya asili ya selous.
Tembo hao walianza kuvamia mashamba ya wakulima kuanzia mwezi watatu mwaka 2019 na kufanya uharibifu mkubwa wa mazao ya wakulima ikiwemo mpunga na mahindi. Aidha nje ya kutaarifiwa mali ya sili wa wilaya hii ya Tunduru kuja kuwatoa tembo hao kwenye makazi ya watu lakini hadi sasa inaonekana wamewashindwa na kuendelea kuchangamana na watu.
Tembo hao kwa sasa wamekuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo kiasi kinachopelekea wananchi kutokufanya shughuli zao za kiuchumi kwa amani kwa hofu ya tembo hao na sasa tembo wamekuwa wakiharibu mikorosho na mbaazi na bustani za mbogamboga.
Tunaiomba serikali itie mkazo katika kuwadhibiti na kuwatoa katika maeneo haya na kuwarudisha hifadhini kabla hawajaleta madhara makubwa kwa binadamu.
Asante.