tunduruboy
JF-Expert Member
- Mar 16, 2013
- 423
- 218
BUNGElimeelezwa kuwa ifikapo mwaka 2020 tembo watakuwa wametoweka nchini iwapo kasiya ujangili wa wanyama hao itaendelea bila kudhibitiwa.
Kwa sasa idadi ya tembo imeelezwa kupunguakutoka 109,000 mwaka 2009 na kufikia 70,000 mwaka jana, hali ambayo inachangiwana ongezeko la ujangili nchini.
Hayo yalisemwa bungeni jana na Mwenyekiti waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli,alipokuwa akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kuhusu makadirio ya mapato namatumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2013/2014.
Lembeli alisema kuwa kwa sasa ujangili watembo nchini umekuwa ni janga la kitaifa ambapo kwa mujibu wa tafitizilizofanywa na Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori zinaonesha kwamba tembowasiopungua 30 huuawa kwa siku, 850 kwa mwezi na kwa mwaka ni 10,000.
"Hali hii ni hatari na aibu kwa nchi yetuambayo ni ya pili barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya tembo,kinachosikitisha ni wizara kuwa na kigugumizi katika kuitikia kauli ya RaisKikwete iliyoitaka wizara kuomba msaada kwake kama tatizo la ujangililimewashinda," alisema.
Alisema ili kunusuru wanyama hao kuweko katikamapori nchini kamati iliiagiza serikali kufanya operesheni kwa nchi nzima nakufanyia marekebisho sheria ya wanyamapori na kuweka adhabu kali kwawatakaothibitika kuhusika na ujangili wa tembo.
Katika hatua nyingine, kamati hiyoilisikitishwa na kitendo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuzuia silahabandarini ikidai kodi, silaha hizo zilinunuliwa na wizara kwa ajili yakufanikisha mchakato wa kupambana na ujangili, hivyo iliiagiza serikalikuruhusu utoaji japo kwa masharti.
Waziri Kagasheki
Awali Waziri wa Maliasili naUtalii, Khamis Kagasheki, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedhaya wizara hiyo alisema katika kuimarisha ulinzi wa wanyamapori zilifanyikajumla ya doria 59,338 ndani na nje ya mapori ambapo jumla ya watuhumiwa 1,215walikamatwa.
Mbali na watuhumiwa hao pia zilikamatwabunduki 85 na risasi 215 za aina mbalimbali, ambapo kesi 670 zilifunguliwakatika mahakama mbalimbali nchini, kati yake 272 zilikwisha na washtakiwa 247 walilipa fainiya sh milioni 175.002 na washtakiwa 71 walipewa adhabu ya vifungo vya miaka 99.
Aidha, kesi 398 zenye jumla ya washtakiwa 897bado zinaendelea katika mahakama mbalimbali nchini ambapo wizara ilifanyaoperesheni ya kiintelijesia wilayani Liwale na Tunduru na kukamata watuhumiwa354, bunduki 435 za aina mbalimbali na risasi 1,129, maganda 514, mbao 10,332na nyara mbalimbali za serikali zenye thamani ya sh milioni 855.014.
Kagasheki aliomba kuidhinishiwa sh bilioni75.6, kati ya hizo sh bilioni 64 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh bilioni11 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Source: TANZANIA DAIMA