Said S Yande
JF-Expert Member
- Mar 16, 2013
- 929
- 745
Tembo ni jumba la wadudu. Wadudu wanaishi humo wakila na kunywa huku tembo akiendelea na maisha yake. Tembo hana uwezo wa kuua wadudu, hivyo kawafanya kuwa rafikize as long as hawamdhuru.
Wadudu wamegundua kuna nyuki na siafu wanamsumbua tembo - nyuki na siafu nao wanatafuta chakula na pa kuishi. Tembo hana hata hizo taarifa.
Mwili ni mkubwa mno kujua nani anang'ata wapi. Wadudu wamekasirika. Wadudu hawataki tembo aguswe. Jumba lao na misosi yao wanaona kama inatishiwa.
Wadudu wameapa watawang'ata nyuki na siafu na kuwamaliza.Wadudu wanasahau kwamba nyuki na siafu ni wadudu wenzao. Wanahofia usalama wao - wanasahau tembo ni mkubwa, wanapambana na wadudu wenzao - wawaue.
Tembo anawashangaa wadudu hawa walio ndugu wanavyouana, ila kwa sababu mapigano hayo hayamdhuru na wala hayampi faida - anawaacha.
Majani yake yapo, mengi tu; maji yake yapo, mengi tu. Kupigana na kuuana kwa nyuki, wadudu, na siafu hakumpunguzii tembo starehe zake.