Telsa Model 3

Telsa Model 3

ng'ombo

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
418
Reaction score
619
Mo Dewji anatarajia kununua gari mpya aina ya Telsa model 3, ambalo linasifika kuwa ni la kiusalama zaidi kuliko mengine yote duniani, linauzwa dola 46,000 (TAS 106,000 Milioni ) Inatumia gesi na umeme tu. Sifa kubwa ya gari hii ni halina muungurumo linatembea kimya kimya, lina camera za dashboard zina uwezo wa kuchukua matukio yote mbele nyuma na pembeni kuzunguka gari na huchukua video zenye ubora wa hali ya juu, yaani HD.
Screenshot_2018-12-24-12-47-39-1.jpeg
 
Ila gari hilo siyo kinga kwa watekaji. Mo ulivyotekwa watu wanapiga dua kila saa. Unapatikana halafu unajifanya kama vile hakuna kilichotokea! .

Kila mtu akitekwa ajiombee mwenyewe huko alipo.
 
kama ni 106,000,000/= mbona ni kidogo sana kwa wenye nazo ukilinganisha na hadhi ya usalama wao!

kama ndivyo, basi akichelewa tu kuwa nayo. pichani ni kama ameshaivuya tayari. au sio hiyo tesla?
 
-Halina injini ni full umeme tu.
-Halitumii ufunguo.
-Haliwezi kuibiwa.
-Haliwezi kugonga.
-Lina automatic brake.
-Linaweza kujiendesha(auto pilot).
Unaweza kuliendesha kwa simu.
-Unaweza kulituma au kuliita kutoka sehemu ya mbali kwa kutumia simu au ipad(kama umecheki movie ya KINGSMEN utakuwa unaelewa).
-Gharama za jumla za kulinunua na kujenga mitambo ya kuchaji ni wastani wa Tsh milioni 250.
 
Back
Top Bottom