Teknolojia mpya ya kuzalisha umeme

Kaka Mkubwa

Senior Member
Oct 10, 2008
154
10
Teknolojia mpya ya kuzalisha umeme.

Teknolojia mpya ya kuzalisha umeme jijini London kwa njia ya matuta ya barabarani (Road Humps) ipo katika majaribio ambayo ni ya kwanza aina yake duniani.
Mamlaka ya Ealing, London imepewa madaraka ya kufanya majaribio hayo kwa kupitisha gari za Polisi juu ya matuta hayo (pichani).
Kila mara gari inapopita juu ya matuta hayo yanakuwa yanasababisha 'pressure' ambayo inazalisha umeme.
Umeme unaozalishwa kwa nguvu ya uzito wa gari yapitayo kwenye matuta, utakuwa unatumika kuendeshea taa za barabarani za usalama (Street Lights, Traffic Lights na Road Signs).
Majaribio hayo yakiwa na matokeo mazuri, teknolojia hiyo itaendelezwa kutumiwa mji mzima wa London.
Muwakilishi wa Ealing alisema, chini ya matuta hayo kuna vitu kama sahani ambazo sahani hizo zinagusana gari inapopita juu na kusababisha nguvu ya umeme.
Kila tuta moja kutengeneza linagharimu £50,000.00 (elfu hamsini), pesa hizo zinalipwa na mamlaka ya usafiri wa London (Transport for London).
Vilevile alisema muwakilishi huyo, matuta hayo yanaweza (kupanda na kushuka) kupandishwa kuwa kama kigezo cha kupunguzia magari kasi au yanaweza kushushwa na hata madereva wasihisi kama wanapita juu ya matuta.
 

Attachments

  • Teknolojia mpya ya kuzalisha umeme.doc
    57 KB · Views: 119
Back
Top Bottom