Mawasiliano yana sehemu tatu: 1) sender 2)medium 3)receiver:
Ukitaka kudukua mawasiliano unaweza ukafanya katika sehemu hizo tatu. End-to-end encryption ina maana hakuna mtu katikati anaweza kufuatilia mawasiliano yenu kwa sababu kabla ujumbe haujatumwa unafungwa(encrypted) na haufunguliwi mpaka ufike kwa receiver(decryption).
Hii whatsup mpya ni tofauti na huduma ya ujumbe wa simu (SMS) ambako kati ya sender na receiver kuna makampuni ya simu. Ujumbe unatumwa kama ulivyo bila kufungwa, unapokelewa na server za makampuni ya simu na baadae kutumwa na server hizo kwa mhusika(receiver). Hivyo ukifuta ujumbe kwenye simu yako au ya anayetumiwa, makampuni ya simu bado yanakuwa na messeji mlizotumiana katika server zao na wanawapatia polisi na vyombo vingine vya dola wakitaka kwa sababu wao wako katikati ya mawasiliano yenu. Hivyo whatsapp ni bora kuliko sms ya kawaida kwa sababu hakuna namna polisi watapata mawasiliano yenu kama sender au receiver hakuwapatia.
So TCRA bado wanakamata kwa sababu receiver anawapatia taarifa zako. Kumbuka kwenye sms za kawaida, hata usipowapatia, bado wataenda Voda,Tigo,Zantel,nk na kuyapata hayo mawasiliano.
Ushauri kisheria:
Ukihisi ujumbe wa whatsup umepelekwa kwa 'wasiohusika':
- Kwanza ufute huo ujumbe/chat nzima baina yako na huyo aliyekutumia
- Ondoa whatsapp katika simu yako
- factory reset
- usimpe email address yako mtu yeyote. Au ukitakiwa kutoa email address-toa tofauti naile uliyojiungia whatapp au uliyotengenezea account ya simu zako. Unique ID ktk smartphone ni email address-sio namba ya simu
Hizi hatua hazimaanishi huwezi kupatikana na hatia-zinafanya wahusika washindwe kuthibitisha 'pasipo shaka' kwamba ulitenda kosa. Kumbuka, number za simu zinaweza kufekiwa (phone number spoofing), pia hata email address zaweza kughushiwa. Naweza kabisa kufungua akaunti yangu ya email kwa jina la Donald Trump na kuitumia bila shida(dtrump@gmail.com). Hivi vitu vinafanya kuthibitisha
pasipo shaka kwamba ulitenda kosa kuwa ngumu.
Wanaokukamata wanatakiwa wa'clone' simu yako na ya huyo aliyesnitch-hawatakiwi kufanyia uchunguzi wao na kuandaa ushahidi kwa kutumia simu halisi kwa sababu kuna uwezekano wa kuharibu ushahidi.