Habari zenu wakuu,
Naomba msaada wenu ktk hili, nimeona post za wadau wakielezea na kutoa juu ya update za simu zao na jinsi zinavyoongezeka ubora wake ktk matumizi.
Je, kwa simu za Tecno zinaweza kufanyika hivyo? Na unafanyaje ili uweze kuupdate simu yako?
Natumia Tecno H6 version ya 4.4.1
Cc Chief-Mkwawa, mwlRCT
Hii haiwezekani, kwa sababu ya chip zinazotumika (Mediatek) haziwezi kusupport firmware na OS updates za simu. Kwa hiyo ukinunua simu ina version fulani, tegemea kuwa na version hiyo hiyo mpaka utakapoamua ununue simu nyingine.
Binaries zinazotolewa na MediaTek ni Closed ended kwa hiyo manufacturers wa smartphones zinazotumia MTK processor hawana uwezo wa kutengeneza OS mpya itakayoendana na Chipset husika.. Hii ni tofauti na Qualcomm ambayo Binary Codes zake ni Open Source kama ilivyo Android OS kwa hiyo giants kama Sony, Samsung, LG na HTC wana uwezo wa kufanya modification ya Android version mpya ili kuendana na Smartphone zao
Baadhi ya tecno zina OTA update, mfano tecno Phantom z, tecno A7 tecno R7 n.k, sasa sijui hizi wanatumia chip gani
Ota ipo kwenye kila simu sababu ni feature ya android, ila kupata hio update ni issue nyengine.
Unaweza pewa update ya apps tupu ikaongeza tu idadi ya apps zako lakini usipate updates ya vitu kama firmware
wanatoa update ya firmware na Android version bro, mfano R7 ilitengenezwa ikiwa na Android 4.2.2 jellybean ila ikapokea OTA update mpaka Android 4.4.1 Kitkat..
Ilitoka lini hio simu?
Habari zenu wakuu,
Naomba msaada wenu ktk hili, nimeona post za wadau wakielezea na kutoa juu ya update za simu zao na jinsi zinavyoongezeka ubora wake ktk matumizi.
Je, kwa simu za Tecno zinaweza kufanyika hivyo? Na unafanyaje ili uweze kuupdate simu yako?
Natumia Tecno H6 version ya 4.4.1
Cc Chief-Mkwawa, mwlRCT
Hii kwenye Tecno H6 ina maana gani?
nadhani ilitoka 2013 mwishoni au 2014 mwanzoni, jaribu ku Google details zake utaipata
Nimeicheki bestmob imetoka april 2014 na kitkat ilitoka around september/october 2013.
Hivyo ilianza kutoka kitkat kabla ya hio tecno.
Hivyo hapo kama ulipata update ya kitkat ujue ulipigwa changa la macho sababu os ilikuwa imeshatoka wakati hio simu ikitengenezwa (miezi 7).
Update inayozungumziwa hapa ni mfano huu.
S4 ilitoka ikiwa na android 4.2 au 4.3 mwanzoni mwa 2013, then ikapata version zote za kitkat mpaka sasa hv ipo lolipop.
Simu ya 2013 inapata update ya 2015 na sio simu ya 2014 inapata update ya 2013