Tecno siyo Simu ya Kujisifia na Kuifananisha Na High Quality Phone

naona wengi mnaikandia tecno especially C8, Hivi mnajua kwamba C8 sio ndio simu ya juu kabisa ya tecno? C8 ina bajeti ya kati ya 280,000/- hadi 250,000/- . sasa basi bei hiyo inaendana na uwezo wake. Hebu sema ni simu gani ya Samsung/HTC/Lumia/Sony/Huawei yenye Specs hizo na inauzwa bei hiyo?

Huawei Y6 iliyokuwa ovyo kabisa ilikuwa 235,000/- na ram yake ya 512.

sasa basi unalinganisha SAMSUNG S4/NOTE3/NOTE4 simu zilizochezea Laki 7 laki 8 na 8 ya 280,000/-

kwanini basi hata usingelinganisha hizo simu zingine na tecno R7 au Phantom Z au Phantom 5. au ulinganishe C8 na hizo simu zenye bajeti zinazokaribiana J1/J2.

Is it fair. tecno ina watumiaji wengi sana afrika almost 50% hivyo lazima matatizo yake yatakuwa mengi.
Dah umeongea bonge la point, yaani kuna watu wanafananisha S7 ya milioni na J8 ya laki 3 sio fair kabisa
 
du kiukwel yang ndo inaelekea kufa...n techno h5. nikipga screen inazima..na hata kukata nashindwa labda niliempigia akate yeye..kuna mda inajibonyeza tu...hata kama sijaigusa....camera ndo shida kabisaaaa
Pole itakuwa una bahati mbaya
 
How come a grownup person can decide to buy techno? Techno = C.C.m
 
Tangu toleo la kwanza android ya tecno n3 mpaka sasa Nina tecno boom j8 sijawah kujuta kitumia iz CM afu sio kwel tecno CM yakeya mwsho n c8 wakat kuna hii boomj8 na c9
 
Tangu toleo la kwanza android ya tecno n3 mpaka sasa Nina tecno boom j8 sijawah kujuta kitumia iz CM afu sio kwel tecno CM yakeya mwsho n c8 wakat kuna hii boomj8 na c9
Mkuu nimetumia sana tecno phantom Z na Z Min. Nimetumia pia H6. Sijawahi jutia kutumia tecno. Sasa hivi natumia kitu cha infinix Hot S ni simu matata ya bei nafuu na ina qualities muhimu nyingi tu ikiwemo4g, finger print, magnetic sensor, 2 GB Ram, Camera 8MP kwa 13 MP na inatoa very high quality pictures kuliko phantom z min ambayo nayo ina 13MP
 
TECNO nilishafunga mkataba nao since 2014/2015 baada ya simu yao kucorrupt internal memory.. Wanakera sana aisee ndani ya miezi miwili au mi3 lazima watoe simu mpya tena ambazo 'most of its feature' ni zilezile.... Ubunifu wao sanasana ni kucopy na kupaste feature za simu nyingine zenye soko zaidi yao na kuzileta huku Afrika ambapo zina soko la watu wa kipato cha chini na cha kati
 
Zama hizi sio zama za kushindana matumizi. Kila uchao simu mpya zinaletwa Africa>Tanzania sisi kazi yetu kununua tu mara iPhone, sijui Galaxy S7 etc
Haya makitu yanatia umaskini tu hakuna kingine zaidi ya show off.
Ukitaka kununua kila model mpya ya sim inayotoka, utashindwa kufanya mambo mengine.
Mi simu yangu inakua na sifa hizi

Ram at least 1GB
Processor 1.2 GHz
Higher android kuanzia kitkat>Lollipop>marshmallow etc
Screen size at least 4.5 inches
Battery capacity iwe angalau 3,000mA
Storage kuanzia 8GB
Camera kuanzia 8 MP rear, front at least 5 MP.
Hapo nimemalza, sitaki kununua sim ambayo ikipotea wiki nzima nasikitika.
Najua siwezi tumia zaidi ya miaka miwili maana itanichosha tu sasa yanini nihangaike na very expensive phone?
Nanunua hiyo ya kawaida tu nikiichoka nauza najichanga nanunua model nyingine
Tatizo wengi hawazijui hizo specifications na zipi ni bora zaidi.
 
Tecno na Infinix walewale tu..hamna kitu kazi kucopy na kupaste features za magwiji kama Samsung, Apple, Huawei,Sony and Htc.
Nakubaliana na ww, lakini wamewawezesha watu wengi kumiliki smartphones zenye ubora kwa bei nafuu. Ukinunua samsung ya laki mbili na nusu unakuta ina ram ya 500 MB na 2000 mah. wakati tekno ya bei hiyo ina Ram ya 1.5gb na betri ya 3000mah. Hapo mtu wa kipato cha chini automatic atachagua simu yenye vigezo vikubwa kwa bei nafuu kuliko kununua simu yenye vigezo vidogo kwa bei kubwa.
Aaidha, Usisahau hata samsung alivoingia alikuwa ignored wakati Nokia kashatangulia kushika soko. Nokia alivojitoa mwenyewe sokoni ndio samsung akapata uwanja wa kutamba, wajanja wote wa mjini walikuwa hawatumii samsung bali nokia. Saivi hao hao walioitosa samsung wanakimbilia samsung kama wamelogwa.
 
mkuu uko sahihi kabisa..
 
Tecno bado kabisa haiwezi kuingia kwenye ligi ya wakubwa hata ukileta Ile high end yao...phantom 6
 
Team Tecno hawata kuelewa kamwe! Mimi visimu ushuzi sijui Tecno Mara Huawei huwa sivigusi bora nitumie Nokia ya Tochi
Huawei wana high end zao ambazo ziko powa sana... Kama honor 8,mate 9 na p8... Huawei wanakuja vizuri
 
Huawei wana high end zao ambazo ziko powa sana... Kama honor 8,mate 9 na p8... Huawei wanakuja vizuri
Me ninachoona kila kampuni ya simu inatoa products zake kulingana na uwezo wake. Kampuni ambazo zimekomaa (kiteknologia na mtaji) huwezi kufananisha na kampuni ndogo. Samsung kuwachapa nokia walitumia nguvu kubwa sana lakini kwasababu walikuwa wamekomaa. Ila nokia nao wamegundua kuwa waliteleza hivyo nao wameanza kutoa android smartphones. Kwa mtazamo wangu linganisha Techno na Huwawei labda. Samsung linganisha na Iphone na Google. Nahisi unaweza kuwa fair.
 
Wateja wingi humu wanaperuzi na techno na wanasoma hii thread vizuri tu kama ulivyoiandika kutumia nini sijui halafu na kesho njoo na nyingine wataisoma na tecno itakuwa mchana kisha usiku
 
Back
Top Bottom