God knows
JF-Expert Member
- Sep 6, 2011
- 276
- 173
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na maswali mengi, ubishani na maneno kwamba Tecno Phantom A na Samsung Galaxy S4 zinafanana na zina uwezo sawa.
Kutokana na hilo, nimeona ni vyema nikazifananisha simu hizi kwa mwonekano na uwezo pia ili kama unataka kununua, ufanye maamuzi sahihi!
Simu zenyewe ndo hizo hapo chini kama unavyoziona kwenye picha!
Kwanza nitaanza kuzifananisha bei.
Tecno Phantom A: Tshs. 358,442.75
Samsung Galaxy S4: Tshs. 935,933.87
Hizi ni bei za makadirio. Bei zinaweza kuwa tofauti kulingana na mahali ulipo na duka pia. Ila kwa wastani, Samsung Galaxy S4 ina bei mara 3 zaidi ya Tecno Phantom A.
Tecno Phantom A ni nene Zaidi kuliko Samsung Galaxy S4. Pia ni nzito na ndefu Zaidi kuliko Samsung Galaxy S4.
Simu zote mbili zina screen za nchi 5. Resolution zake zipo kama hivi:
Tecno Phantom A: 1220 X 720
Samsung Galaxy S4: 1920 X 1080
Tofauti inapokuja kati ya hizi simu mbili ni Teknolojia iliyotumika katika kutengeneza screen zake. Samsung Galaxy S4 ina Super Amoled Screen wakati Techno Phantom A inatumia TFT Technology. Hii inamaanisha kwamba Display ya Samsung ipo sharp Zaidi. Ila kama haupo sensitive sana, ni ngumu kuona utofauti katika mwonekano wa vioo vya simu hizi.
Sasa ngoja tuongelee Camera za simu hizi zote mbili:
Samsung Galaxy S4:
Tecno Phantom A:
Sasa ni vyema tukatazama Operating Systems kwenye simu zote mbili. Simu zote hizi ni za Android 4.2. Ila Samsunga Galaxy S4 inakuja na Android 4.2.2 na Tecno Phantom A inakuja na Android 4.2.1.
Android inayopatikana kwenye Samsung Galaxy inakuja na Features & Customizations nyingi ambazo zimeongezwa ambazo hizo zinaipa look na feel ya Samsung.
Kwa upande wa pili, Android ya kwenye Tecno Phantom A, inakaribia kuwa sawa na Android Halisi inayotolewa na Google. Hawajafanya customizations ili angalau ilete mwonekano wa Ki-tecno Zaidi. Labda kwenye matoleo yajayo itafanyiwa marekebisho ingawa hata sasa bado inaonekana kuwa sexy!
Technical Specifications:
Tecno Phantom A:
Tecno Phantom ina Dual – Core Processor ambapo kila Core ina 1.2 GHz. RAM yake ni 1GB. Uwezo huu kwa simu ni wa kawaida na ni mzuri pia kwa shughuli za kila siku. Pia inafaa kwa kuchezea ma-game mazito kwa wale gamers.
Samsung Galaxy S4:
Kwa upande wa Samsung Galaxy S4, uwezo wake huku ni amazing. Ina processor yenye 8 cores. Cores 4 za kwanza kila mmoja ina uwezo wa 1.6 GHz na Cores 4 zinazobaki kila mmoja ina 1.2 GHz. RAM yake ni 2GB.
Specifications hizi ni Zaidi ya mahitaji ya simu. Sijui kama kuna Application yeyote ya simu duniani inayohitaji simu ya uwezo mkubwa kiasi hiki. Mimi naweza kusema ni wastage na labda ndo inayochangia simu hii kuwa na bei kubwa.
Kuwa na simu hii ni sawa na kubeba Computer kubwa na kutembea nayo barabarani!
Note: Kwa wageni kwenye teknolojia.
Tunaposema Processor ina Dual Core Processor, tunamaanisha kwamba ndani ya processor moja, kuna vi-processor vidogo viwili. Hii ina maana kwamba kupata speed kuu ya simu yako, unazidisha hiyo 1.2 kwa Tecno mara 2.
Kwa maana hiyo hiyo, Samsung Galaxy S4 ina vi-processor 8 ndani yake.
Hitimisho:
Nikitakiwa leo kununua simu, basi nitanunua Tecno Phantom A. Hii ni kwa sababu inafanya vitu vyote ambavyo Samsung Galaxy S4 inafanya. Pia inapatikana kwa bei ndogo na inaruhusu kuweka line 2 kwa wakati mmoja.
Kwa mtazamo wangu, kumiliki Samsung Galaxy S4 ni sawa na kuchezea hela. Labda kwa wale ndugu zangu akina Ngosha na Wahaya ambao kuwa na kitu cha gharama kunamaanisha High Status, hawa inawafaa hii Samsung Galaxy S4!
Nawasilisha.

- Camera ya nyuma in 13 MegaPixel na inaweza ku-record video katika full High Definition. Ya mbele ina 2 MegaPixel.
- Software ya Camera imeongezewa features nyingi pia.
Tecno Phantom A:
- Camera ya nyuma ina 8 MegaPixel na ya mbele ina 1.2 MegaPixel. Camera hii ya nyuma inauwezo sawa na Camera zinazopatikana kwenye simu maarufu kama vile IPhone 4s, 5s na 5c. Sio mbaya kwa matumizi ya kawaida ingawa quality inakuwa chini kidogo ukifananisha na picha iliyopigwa kwa Samsung Galaxy S4.
- Software ya Camera ni ya kawaida ambayo originally inakuja kwenye Android bila features zozote zilizoongezwa.