Eric Mkomoya
Member
- Oct 10, 2014
- 55
- 56
Katika kampuni za simu, Tecno ni kampuni bomba inayojali wateja wake na ndio maana tunawaelekeza wateja na watumiaji wote wa bidhaa za Tecno, kumekuwa na maneno ya upatu kuhusu simu za Tecno kuwa bandia, lakini upatu hauwezi kubadilisha uhalisia wa Tecno usiogope, jiamini, amini Tecno, usiandikie mate na wino ungalipo, Kamwe Tecno hazitafungwa kupitia TCRA. Hapa kuna hatua za kufahamu kama simu yako ni orijino au la, simu iliyotumika hapa ni Tecno C8.
Hapo tayari, simu inaonekana kuwa ni orijino kwani ina jina la mtengenezaji ambaye ni kampuni ya Tecno yaani Tecno Telecom Limited na aina ya simu ni Tecno C5. Furahia bidhaa za Tecno kwani zimeenea karibu nchi zote Afrika, Ulaya na Asia.
- Andika *#06# kisha bonyeza kitufe cha kupiga
- Baada ya hapo simu yako itakuletea IMEI namba, ambapo kama simu yako ina laini mbili basi zitakuja IMEI namba zikiwa mbili, lakini unapaswa kutumia mojawapo kati ya hizo mbili. Kama zinavyoonekana hapo chini.
- Namba hii pia unaweza kuipata nyuma ya simu ukitoa betri na utaijua kwani huwa na tarakimu 15, kwa simu zisizohamishika betri namba hizo utazipata mwanzoni ukishatoa mfuniko wa simu yako.
- Nakili namba hizo pembeni.
- Iandike ile namba kwenye sehemu ya kuandikia ujumbe(message)
- Utume ujumbe huo kwenda namba 15090, kama inavyoonekana kwenye picha.
- Baada ya kutuma jumbe, utaangaliziwa aina ya simu na mtengenezaji, mfano Tecno Telecom Limited na aina ya simu ni C5.
- Subiri majibu kwa ujumbe mfupi haitachukua muda.
- Ujumbe huo ukija unakuwa na Kampuni iliyotengeneza simu hiyo pamoja na aina ya simu basi ujue simu yako ni orijino kama inavyoonekana hapo chini.
Hapo tayari, simu inaonekana kuwa ni orijino kwani ina jina la mtengenezaji ambaye ni kampuni ya Tecno yaani Tecno Telecom Limited na aina ya simu ni Tecno C5. Furahia bidhaa za Tecno kwani zimeenea karibu nchi zote Afrika, Ulaya na Asia.