real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Mtandao wa kutokomeza ndoa za utotoni TECMN umewashangaa baadhi ya wabunge waliopinga watoto waliopata ujauzito kurudi shuleni na kusema hilo linadhihirisha hawatambui viini vya matatizo yaliyopo katika jamii.
Wamesema watoto wana haki ya msingi ya kupata elimu haki yake ya msingi na kumnyima fursa hiyo kwa kigezo cha ujauzito ni ukiukwaji wa haki za mtoto na haki za binadamu ambazo Tanzania imesaini.
Wamesema tafiti zinaonyesha zaidi ya 27% mwaka 2015 ya wasichana wenye miaka kati ya 15-19 ikiwa imepanda kutoka 23% mwaka 2010 huku mjini 19% kukiwa ni na vijijini ikiwa ni 32% na mikoa inayoongoza ikiwa ni Katavi 45%, Tabora 43% Dodoma na Morogoro 39% , Mara 37%, Mbeya 32%.
Na kitendo cha wabunge kinazidi kudidimiza haki ya mwanamke, ndoa za utotoni na kuzidisha umasikini.