Tec yawashangaa ukawa

Tec yawashangaa ukawa

Mdachi Simple

Member
Joined
Aug 20, 2014
Posts
11
Reaction score
3
TEC YAWASHANGAA UKAWA

Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa
Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu
Severine Niwemugizi, alisema Ukawa
walikuwa na kikao cha maridhiano na Rais
Kikwete, hivyo walikuwa na nafasi ya
kumtaka asitishe Bunge.
Alisema badala yake walitoka kwenye kikao
hicho na kuanza kulalamikia wananchi
huku wakiwaambia waandamane ikiwa Rais
Kikwete atashindwa kusitisha shughuli hizo.

“Inashangaza kuona Ukawa wanalalamika
nje ya kikao wakati walikuwa na nafasi
kubwa ya kumwambia Rais Kikwete asitishe
Bunge mara baada ya kumalizika kwa kikao
chao, badala yake wameamua kuja kwa
wananchi na kuanza kulalamika.

“Kwani katika hicho kikao hawakuwa na
makubaliano? Na kama ni hivyo kwanini
walikubali kutumia Katiba ya mwaka 1977
kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
na Uchaguzi Mkuu mwakani?” alihoji.

Alisema katika kikao hicho Ukawa na Rais
Kikwete waliingia makubaliano ya kusitisha
mchakato wa Bunge hadi mwaka 2016 ikiwa
Rais ajaye atakubali kuendelea nao.

“Nimewashangaa sana wajumbe wa Ukawa,
kwa sababu walikuwa na nafasi kubwa ya
kuwasilisha malalamiko yao kwa Rais na
kuingia makubaliano ya kusitishwa kwa
shughuli hizo, lakini baada ya hapo
wanakuja kwa wananchi na kuanza
kulalamika huku wakidai kuitisha
maandamano, kwani hawakuwa na nafasi
ya kumwambia rais malalamiko yao,”
alisema.
 
Amesema kama Tamko Rasmi la TEC au ni mawazo yake binafsi?
 
UKAWA walisema wataandaa maandamano "nchi nzima" yaliishia wapi?
 
Back
Top Bottom