Mdachi Simple
Member
- Aug 20, 2014
- 11
- 3
TEC YAWASHANGAA UKAWA
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa
Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu
Severine Niwemugizi, alisema Ukawa
walikuwa na kikao cha maridhiano na Rais
Kikwete, hivyo walikuwa na nafasi ya
kumtaka asitishe Bunge.
Alisema badala yake walitoka kwenye kikao
hicho na kuanza kulalamikia wananchi
huku wakiwaambia waandamane ikiwa Rais
Kikwete atashindwa kusitisha shughuli hizo.
Inashangaza kuona Ukawa wanalalamika
nje ya kikao wakati walikuwa na nafasi
kubwa ya kumwambia Rais Kikwete asitishe
Bunge mara baada ya kumalizika kwa kikao
chao, badala yake wameamua kuja kwa
wananchi na kuanza kulalamika.
Kwani katika hicho kikao hawakuwa na
makubaliano? Na kama ni hivyo kwanini
walikubali kutumia Katiba ya mwaka 1977
kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
na Uchaguzi Mkuu mwakani? alihoji.
Alisema katika kikao hicho Ukawa na Rais
Kikwete waliingia makubaliano ya kusitisha
mchakato wa Bunge hadi mwaka 2016 ikiwa
Rais ajaye atakubali kuendelea nao.
Nimewashangaa sana wajumbe wa Ukawa,
kwa sababu walikuwa na nafasi kubwa ya
kuwasilisha malalamiko yao kwa Rais na
kuingia makubaliano ya kusitishwa kwa
shughuli hizo, lakini baada ya hapo
wanakuja kwa wananchi na kuanza
kulalamika huku wakidai kuitisha
maandamano, kwani hawakuwa na nafasi
ya kumwambia rais malalamiko yao,
alisema.
Anajuawaje hawakumwambia! Kama alikataa kuwakbalia anataka nao wanyamaze eti tu kwa kuwa walikuwa na kikao na raisi! Huyu asikofu wa jumbo LA rulenge-ngara c ndiye aliyetoa tamuko LA kuwalaan ukawa akiwa na pinda pale iringa? Nani haju msimamo wa huyu askofu? Hawa ndo tunaita mkanjanja hawa! Ukimusikia redio kwizera tu utagundua huyu no MTU wa namna gani! Na yuko upande UPI! Tafadhari asitumie mwvuli wa uaskofu kwa. Masilai ya chama chako.kuwa makini na kauli zako wewe no kiongozi wa wananchi wenye itikadi tofaiti! Be care askofu usijiingize kwenye migogoro bure kwa kusaka vyeo,pesa na huruma za watawala eti tu uonekane mwena!
Muumini wako jumbo LA lulenge-ngara kagera
Lengo la ukawa ni kutuletea vita,watafanya jitihada zote ili wafanikiwe.
Yes yeye ndiye msemaji wa TEC hutaki unaacha ukawa hawajitambui.Kwani huyu Askofu ndio msemaji wa TEC??!! Acheni kuchafua imani za watu kwa kutumia mawazo ya mtu mmoja ambayo sio official....Huyu askofu ameeleza mawazo yake kwa mapenzi ya lichama lake na sio msimamo wa TEC.....Huyu ni kama yule askofu mwingine alisemaga "Kikwete ni chaguo la Mungu". matokeo yake leo hii yuko wapi?? kutoka Askofu msaidizi wa JIMBO KUU DSM hadi askofu wa kawaida huko jimboni kwake kwa mishomire......CHEZEA KANISA WEWE!!!!
Kusoma siyo kuelimika mkuu wapo wasomi wengi ambao hawajitambui wanachofanya.ukawa wamanikera kwelikweli usomiwao upo wapi sasa
Yes yeye ndiye msemaji wa TEC hutaki unaacha ukawa hawajitambui.
ukawa wamanikera kwelikweli usomiwao upo wapi sasa
TEC YAWASHANGAA UKAWA
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Severine Niwemugizi, alisema Ukawa walikuwa na kikao cha maridhiano na Rais Kikwete, hivyo walikuwa na nafasi ya kumtaka asitishe Bunge. Alisema badala yake walitoka kwenye kikao hicho na kuanza kulalamikia wananchi huku wakiwaambia waandamane ikiwa Rais Kikwete atashindwa kusitisha shughuli hizo.
"Inashangaza kuona Ukawa wanalalamika nje ya kikao wakati walikuwa na nafasi kubwa ya kumwambia Rais Kikwete asitishe Bunge mara baada ya kumalizika kwa kikao chao, badala yake wameamua kuja kwa wananchi na kuanza kulalamika.
"Kwani katika hicho kikao hawakuwa na makubaliano? Na kama ni hivyo kwanini walikubali kutumia Katiba ya mwaka 1977 kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani?" alihoji. Alisema katika kikao hicho Ukawa na Rais Kikwete waliingia makubaliano ya kusitisha mchakato wa Bunge hadi mwaka 2016 ikiwa Rais ajaye atakubali kuendelea nao.
"Nimewashangaa sana wajumbe wa Ukawa, kwa sababu walikuwa na nafasi kubwa ya kuwasilisha malalamiko yao kwa Rais na
kuingia makubaliano ya kusitishwa kwa shughuli hizo, lakini baada ya hapo wanakuja kwa wananchi na kuanza kulalamika huku wakidai kuitisha maandamano, kwani hawakuwa na nafasi ya kumwambia rais malalamiko yao," alisema.