Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 440
- 3,211
Baraza la Maaskofu la Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) limesema Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 imeliingiza Taifa katika hali ya maandamano yaliyozaa vifo, watu kujeruhiwa, kupotea na uharibifu wa mali, hali ambayo imepelekea Taifa kuwa kwenye masononeko, na maumivu kwani wapo walioawa na kuumizwa wakiwa nyumbani kwao bila kuhusika kwenye maandamano hayo
Rais wa TEC Askofu Wolfgang Pisa ameeleza hayo wakati akisoma tafakuri ya pamoja ya Maaskofu wa Kanisa hilo, kufuatia tafakari na sala walizofanya kwa takribani siku nne (4) kuanzia Novemba 11 hadi 14 mwaka huu, ambapo Maaskofu hao wametumia siku hizo kuiombea nchi amani kufuatia mapito magumu inayopitia nchi kwa sasa, kutokana na kile walochokitaja kuwa 'maumivu' waliyonayo Watanzania
Sambamba na kulaani matukio hayo, TEC imesema Taifa limejeruhiwa na kupoteza heshima yake kimataifa ambapo mataifa, hivyo kutumia nafasi hiyo kutoa rai kwa mamlaka husika hususani Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Serikali kwa ujumla kuchukua hatua za haraka za kuliponya Taifa
Wametaka kufanyika uchunguzi utakaoshirikisha wadau wa ndani na nje ya nchi, na kwamba wachunguzi wawe kutoka kwenye vyombo visivyofungamana na upande wowote ikiwemo Taasisi za Dini, Taasisi za Kimataifa huru nk, huku wakitoa wito kwa viongozi wa umma kuishi maisha ya uadilifu na uwajibikaji kwa viongozi
TEC pia imetaka wote waliokamatwa kwa hila kabla, wakati na baada ya uchaguzi waachiwe huru bila masharti yoyote
Aidha, katika maelezo yake, Askofu Pisa amesema tathmini inaonesha kuwa maandamano yaliyotokea nchini yametokana ukosefu wa usalama nchini hasa uwepo wa matukio ya utakaji, kupotea na kuumizwa kwa watu, uwepo wa watu wasiojulikana ambao wamedai kuwa wanaonekana kuwa na nguvu kuliko vyombo vya Dola nk,
Sababu nyingine ni kukosekana kwa demokrasia ya kweli, hasa kilio cha muda mrefu tangu mwaka 2016, kilio ambacho hakijapatikana suluhisho la kweli
Pia, imeelezwa kuwa wananchi wamekosa eneo la kufikisha malalamiko yao pale haki zao zinapokiukwa nk.
Kwa muktadha huo, TEC imeshauri mamlaka husika kuhakikisha inaliponya Taifa na kuhakikisha mchakato wa Katiba Mpya unaanza haraka iwezekanavyo, huku Watanzania kwa ujumla wake wakipewa wito wa kuendelea kusali na kuliweka Taifa kwenye hali ya uponyaji.