TEC hizi tetesi ni za kweli?

TEC hizi tetesi ni za kweli?

macho_mdiliko

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2008
Posts
28,230
Reaction score
56,858
Kuna ndogo ndogo (tetesi) zisizo rasmi (nasisitiza tena... zisizo rasmi) kuwa Ikulu inahaha na uongozi wa juu wa TEC na wale wengine ili utoe tamko kuwa jina aliloteua rais Kikwete la mjumbe TEC kwenye tume ya katiba lilipitishwa na uongozi wa juu wa TEC!

Tamko linatakiwa liseme kuwa uongozi wa juu wa TEC ulifanya ''marekebisho'' kwenye listi iliyokuwepo mwanzoni kabla ya kupeleka majina kwa rais.....

Lengo ni kuwa ionekane Lissu ni mwongo, mzushi na mzandiki kama ilivyosemwa.....

Let us stay tuned....

PS: Kwasababu ni tetesi means unaweza kuwa uongo wa mchana kweupe, hivyo tusitoe lawama kwa TEC wala Ikulu!
 
SSM kazi ipo!!! Kwa nini mnalazimisha watanzania kuishi maisha ya kidikteta? Acha watanzania waamue wanachokitaka, wana akili kwa sasa si wale wa zamani mliowakanyaga kila kitu ni force tu!!!! Mtahangaika wee, na mwadhama Pengo ukikubaliana na hii issue kama ni ukweli basi utakuwa katika kundi la wasaliti wa kanisa.
 
Huu ni uzushi uliopitiliza. TEC haiendeshwi kama lile Baraza kuu letu Tanzania. Ni vigumu kwa TEC kufanya huo ujinga, hata serikali inatambua ugumu wa kuwashawishi TEC wakubali huo utumbo. Ingekuwa baraza kuu au taasisi au shura hapo ingekuwa sawa
 
Ukishazoea kupokea fedha chafu za Michango na harambee kutoka kwa Wanasiasa Mafisadi mwisho wake huwa ndio huo wa kuwa mateka.Ninawasifu Waislamu na Baraza lao la Maulemaa kwani walikataa kabisa kuwa Watumwa wa hawa Mafisadi.TEC is a major disappointment to all of us.
 
Mtu yeyote wa TEC akihusika kufanya matakwa ya wanasiasa ataadhibiwa vikali.
 
Ukishazoea kupokea fedha chafu za Michango na harambee kutoka kwa Wanasiasa Mafisadi mwisho wake huwa ndio huo wa kuwa mateka.Ninawasifu Waislamu na Baraza lao la Maulemaa kwani walikataa kabisa kuwa Watumwa wa hawa Mafisadi.TEC is a major disappointment to all of us.

Mkuu kumbuka nimesema ni tetesi, na kisha bado haijulikani kama TEC watakubali kama hizi tetesi ni za kweli! Usiwahukumu!
 
[MKUU UTAKUWA UMEMSAHAU SHEIKH ABDALLAH PALE MWANZA NA 500m cash money.]
 
Mkuu kumbuka nimesema ni tetesi, na kisha bado haijulikani kama TEC watakubali kama hizi tetesi ni za kweli! Usiwahukumu!

Waambie mods wafute huu uchafu wako. Ukishajiridhisha usahihi wa hizo habari uje uanzishe thread. Tec ni taasisi imara, yenye heshima na ina nguvu kuliko hata serikali yako. Huwezi kuihusisha TEC na tetesi zako za kipuuzi halafu ukataze watu wasiwe huru kuchangia kisa umesema ni tetesi.
Naiona thread yako imekosa maana
 
TEC wanaweza kukubali ni suala la fwweza tu. Ukija na hela mfuko wa shati wanabadilisha maamuzi
 
Wote tunajua kuwa ungekuwa uongo wangekuwa wameriakiti mara moja kama walivyoafanya kwa dr Slaa. Kwa zaidi ya 2000% hizi ni habari sahihi. Haiwezekani tangu mambo haya yazungumzwe Bungeni mpaka leo kama ni uongo hata taasisi moja isiwe imetoa tamko!!!!?!
 
Duh nawaamini hawa jamaa hata km sinaukaribu nao but wamesimama hawawezi kukubali ujinga km huo, wengi wao ni wasomi wanajua nini wanaongea
 
Ukishazoea kupokea fedha chafu za Michango na harambee kutoka kwa Wanasiasa Mafisadi mwisho wake huwa ndio huo wa kuwa mateka.Ninawasifu Waislamu na Baraza lao la Maulemaa kwani walikataa kabisa kuwa Watumwa wa hawa Mafisadi.TEC is a major disappointment to all of us.

You must be sick.Unafikiri TEC ni sawa na lile baraza kuu na taasisi zake? TEC viko vichwa vyenye elimu ya hali ya juu ya kuweza kuchambua na kupambanua mambo mazito,hakuna kuhongwa ubwabwa pale.Tenauwe na adabu na TEC manake ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi hii katika elimuna afya.Mmekalia kulalamika miaka yote,ovyo kabisa!!
 
Kwa sababu ni tetesi basi hali tete, teteteeeeeeeeeeee
 
basai hii inaonesha JK alikuwa analopoka, maana ukweli hauhitaji kupangiwa mipango, wala wasipoteza muda hotuba imekuwa ni aibu kubwa kwa mkuu wa kaya. hata kama lisu angekuwa muongo, mkuu wa kaya likosea kuazima maneno ya mama mtilie kuyatumia kuhutubia taifa...ni aibu isiyo jadilika!
 
Hivi mnaijua vizurinTEC au mnaisikia tu. Ile ni institution iliyokamilika. Haiendeshwi kama zile taasisi za mifukoni. Pita kidogo pale makao makuu Kurasini utajua walau kidogo how it operates!
 
Back
Top Bottom