Team Lowassa nawaambia hivi; Rais Kikwete hatabiriki

Ole Shider

Member
Joined
Oct 17, 2014
Posts
16
Reaction score
15
Asalaam Alekhum Warakhmatulai Wabarakatum;

Katika miezi hii na mwaka tunaoutazamia kumekuwa na maneno mengi, hisia nyingi na matamanio mengi hasa katika kambi mbali mbali za wale wanaojitadi ama kunadiwa kuutaka uongozi.

Naandika haya kwa uchungu sana hasa nikizingatia namna ambavyo Vijana wengine wametumika kutukana watu pasipo sababu za msingi tena wanaotukanwa ni wazee wenye heshima katika Taifa hili.

Sijui sana kuhusu Katiba ama namna ambavyo maadili katika vyama vya Siasa hapa Nchini zinavyoshughulikiwa. Lakini kimsingi hata kama Kanuni zenu ziko silent hivi kweli hata Medula hazifanyi kazi? Taifa hili watu wamelelewa kwa nidhamu, heshima, utu na kuvumiliana lakini hili limekuwa gumu hasa kwa vijana.

Katika kuandika haya nimeona kidogo nigusie utafiti uliowekwa hadharani majuzi ambao umesababisha wale wote waliotamani kuongoza na wameshindwa wameamua kuupinga hadharani bila sababu za msingi.

Niseme tu nami nimebahatika kwenda shule kidogo binafsi nimewashangaa sana wote waliojitokeza hadharani tena wengi wakiwa wasomi na kuupinga utafiti huo. Ule ni upuuzi mkubwa. Watu wanajitoa ufahamu na kujifanya illitirate tena wasio na vision.

Mi niseme wote huo ni uoga...... ShakeSpeare aliwahi sema "COWARDS DIE MANY TIMES BEFORE THEIR DEATH." Imani yangu inanituma kuamini kuwa ni uoga tu ndio unaowasumbua hakuna kingine. Kimsingi Tafiti hupingwa kwa utafiti na ndio msingi wa msingi wa slogan ya "NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK (Mao Tse-Tung)" na si hullabaloo za hapa na pale.

Haiwezekani msomi ukapinga wasomi wenzio kisa ulichotaka wewe kiwe hakijakuwa its very ridiculous. Tunabemenda elimu kwa majibu ya Kiasa ni lazma mjue baada ya siasa bado utabakiwa na taaluma yako unless hiyo elimu iwe ni ya kununua. Mimi swali lililonitatiza mpaka kuamu kufanya utafiti kidogo na kuandika hapa hasa kutokana na utafiti wa TWAWEZA ni jambo moja tu kinachoelekea kupingwa sana ni mtu kuongoza je lile la Chama kukubalika vpi??

Naudhika na kukereka sana pale watu wanapotumia taaluma na muda wao kufanya jambo flani halafu sisi tunakuja na kuwajibu kwa uwepesi tu na ninyi tumeni watu wenu wakatafiti baada ya hapo wekeni mambo mezani kalamu na vitabu vipingane si midomo midomo tu......

Leo nami nizungumze na wanao muungana mkono yule alionesha kuongoza katika tafiti za twaweza... Kwanza niseme tafiti hizi zipo kwa ajili kwa kutuonesha wapi tulipo na zisiwasababishe kusema haya sasa tukae na tunywe kwa kuwa Lowassa kashinda la hasha! Jipongezeni ila oneni kama ndo kwanza mmemwagiwa petroli.

Mna majukumu kadha wa kadha kama yafuatayo;

Mimi ni mmoja kati ya watanzanaia walio wengi wenye kukubali kwa 100% kwamba JK hatabiriki hilo sina shaka nalo hata kidogo. Kama JK anatabirika angetabirika kipindi kile cha Urais wa Zanzibar pale familia yake na wengi walipokuwa wakimuungana mkono Waziri Kiongozi Shamsi Vuai ile yeye (JK) akachomoka na Raisi aliyeko madarakani hivi sasa. Kama JK anatabirika basi angetabirika kipindi cha Tume ya Katiba hakuna namna tume ingefanya kazi isipeleke ripoti kwa Raisi lakini kule Bungeni mliona jamaa alichomfanya Warioba.

Kama JK anatabirika basi angetabirika na baadhi ya Mawaziri aliokuwa nao hakuna anayeamini mpaka leo Dk. Nchimbi ama Kagasheki wangekuwa nje ya Baraza la Mawaziri leo hii. Kama JK anatabirika hata kwa hawa MaRC angetabirika nako manake humu kuliwahi kuletwa uzi kwamba RC wa Arusha asingekaa ahame eti kisa Rais alimuahidi kuzeekea Arusha leo imekuwa je??

Si hivyo tu hata uhamisho wa Makatibu wa ngazi ya Mikoa ndani CCM umeonekana kuwaudhi walio wengi hasa wale waliowahi kujinasibu kuwa wao na bwana mkubwa ni kama mate na ulimi lakini leo wako wapi? Binafsi naamini si familia yake ama mtu mwingine yeyote anaweza kumtabiri JK he is very reserved na watu wamekuwa wakimsingizia sana...... JK ana yake mwenyewe ambayo wengine wameishia kumlisha maneno.

Nimepata kualikwa kwenye kakikao flani cha siri nami nikapelekwa kama mjumbe wa Mkutano ambao wanauita kuwa ni wa CCM Taifa nashukuru manake nilipatiwa changu ktk kile kikao nilichoshangazwa nacho hoja kubwa wanasema JK atamkata Lowassa jina hivyo yeye atashinda like seriously yaani kumbe wengi wanangoja kushindia uji wa matanga. Kwamba Lowassa ni perfect ana vigezo vyote ila kasoro ni kwamba atakatwa jina! Unajua niliona kama naota.....

Nataka niwaambie ninyi mlio wa Lowassa;

1. Nendeni mkawathibitishie watu kuwa Lowassa na JK hawajawahi kuwa maadui na hawana ugomvi. Na JK akate jina la Lowassa kwa lipi?? Na alilisema wapi hilo?? Ndo yale yale nilisema No research....... Wamwache JK waje na yao yenye tija na hoja za msingi.....

2. Nendeni ama endeleeni kuongeza marafiki hakuna haja ya kutengeza maadui wakati huu......

3. Nendeni mkaoneshe tofauti iliyopo kati yenu na wenzenu katika kutetea hoja kwa hoja na si hoja kwa matusi, katika kutafuta kura, katika vitendo na matendo yenu, katika kuendelea kuwasaidia Watanzania hata kama Lowassa kafungiwa.

4. Nendeni mkampongeze JK kwa kazi nzuri aliyoifanyia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si kuwa kama wale wanaozungumza hovyo juu ya taasisi yake.....

5. Nendeni (mimi nadhani ndivyo ilivyo) mkawaeleze watu juu ya Uvumilivu wa Lowassa ndani Chama chenu. Ni nani mnaweza leo kumfananisha na Lowassa linapokuja kwenye swala la Uvumilivu manake kwa zahama aliyopitia hata ingekuwa ni mimi ningeshawaambia to hell with your party au kama alivyowahi kusema Nyerere CCM si baba yangu wala mama yangu. Lakini huyu Mamvi bado kang'ang'ana tu..... Yaani hata haya mpaka muuambiwe.....

6. Kuna mambo ya Kipuuzi puuzi tu eti anaumwa jamani Lowassa wenu ndani ya CCM ni wa kwanza kuzushiwa magonjwa??

7. Oooh mwalimu alimkataa imeandikwa wapi hiyo? Lakini hivi kwani ninyi hamjui kuwa mwalimu aliukataa ubadhirifu? Tena wakati huo kina Pinda wakiwa wasaidizi wake leo hii Nchi mnaona je??

7. Ooh kuhusu kashfa uwajibikaji na kashfa are incompatible words..... Waambieni watu..... Na hili subirini mlizungumzie vizuri baada ya mzigo wa IPTL kutema mawe.....

Kuna rafiki yangu hapa ananiambia nimalizie kwa kusema No Lowassa No CCM kazi kwenu........

Ntaendelea
 
Hii staili uliyokuja nayo nimeipenda,Ni kama unauma huku unapuliza.......werevu tumejua uliposimamia......tunasubiri mwendelezo wake.
 
Haya sifongo. Swaga zako zinadunda wapi?
 
Naudhika na kukereka sana pale watu wanapotumia taaluma na muda wao kufanya jambo flani halafu sisi tunakuja na kuwajibu kwa uwepesi tu na ninyi tumeni watu wenu wakatafiti baada ya hapo wekeni mambo mezani kalamu na vitabu vipingane si midomo midomo tu......

Kwenye maneno niliyoweka red umejivua nguo jamaa yangu...

Kusema "na" ninyi tumeni, it means nyie mlituwatuma TWAWEZA. Ungesema tu "nendeni mkafanye utafiti pia" au hata "tumeni watu wakafanye utafiti pia" Ingeeleweka vingine.

Sasa hakuna mtu mwenye hela za kuchezea kama nyie. Lowassa si ameshinda? Aende basi ikulu kesho...

Tutakutana kwenye sanduku la kura...
 
Umeongea vizuri tu. Ila hapo kwenye No Lowassa no CCM umekosea mno. Kama mnaamini hivyo then u are up to surprise. CCM sio mtu mmoja. Waulize kina Kambona, Mohammed Babu, Edwin Mtei, Horace Kolimba, Kighoma Malima, Lyatonga Mrema, Wilbroad Slaa. NK. Majina ni mengi. Mamvi analijua hilo na ndio maana atafia CCM.

Kuhusu Lowassa kuwa mgonjwa nadhani hilo lisiwe mtaji wa siasa. Wahenga walisema mficha moshi, moto utamuumbua.

kuhusu ufisadi. Well, Lowassa ni fisadi. Lakini kuanzia 2010 mmejisafisha, na kwa kiasi kikubwa kashfa hazijaongelewa. Ila naamini kipindi cha kampeni rekodi yake kuanzia AICC itawekwa wazi. Na waTanzania wataijadili kwa kina. Hilo nakuhakikishia.
 
Kwenye maneno niliyoweka red umejivua nguo jamaa yangu...

Kusema "na" ninyi tumeni, it means nyie mlituwatuma TWAWEZA. Ungesema tu "nendeni mkafanye utafiti pia" au hata "tumeni watu wakafanye utafiti pia" Ingeeleweka vingine.

Sasa hakuna mtu mwenye hela za kuchezea kama nyie. Lowassa si ameshinda? Aende basi ikulu kesho...

Tutakutana kwenye sanduku la kura...
Hilo liko wazi kuwa Twaweza walitumwa na walifadhiliwa na Lowasa. Unabisha?
 
Umeongea vizuri tu. Ila hapo kwenye No Lowassa no CCM umekosea mno. Kama mnaamini hivyo then u are up to surprise. CCM sio mtu mmoja. Waulize kina Kambona, Mohammed Babu, Edwin Mtei, Horace Kolimba, Kighoma Malima, Lyatonga Mrema, Wilbroad Slaa. NK. Majina ni mengi. Mamvi analijua hilo na ndio maana atafia CCM.

Kuhusu Lowassa kuwa mgonjwa nadhani hilo lisiwe mtaji wa siasa. Wahenga walisema mficha moshi, moto utamuumbua.

kuhusu ufisadi. Well, Lowassa ni fisadi. Lakini kuanzia 2010 mmejisafisha, na kwa kiasi kikubwa kashfa hazijaongelewa. Ila naamini kipindi cha kampeni rekodi yake kuanzia AICC itawekwa wazi.
Nakubaliana na wewe mkuu
 
Hivi hili fisadi Lowasa limechangia kiasi gani kwenye ujenzi wa maabara na ununuzi wa madawati? Au fedha zake anazitumia kuwah.onga tu wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM?
 
Kuna waziri alimtangaza OLE SENDEKA kuwa alifeli f4 alipata alama ya YAI, Sendeka anasubiri kumnyamazisha msomi namba moja TANZANIA kwa kumwambia OUT
 
Yaani Sendeka aliyefeli form four aoneshe hasira zake kwa Prof Muhongo? Atakuwa na hoja gani za kuongea dhidi ya prof?
 
JK tutamkumbuka tu, huyu ni Rais wa aina yake katika JMT. Binafsi namfagilia sana
 
Hivi hili fisadi Lowasa limechangia kiasi gani kwenye ujenzi wa maabara na ununuzi wa madawati? Au fedha zake anazitumia kuwah.onga tu wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM?
we umechangia kiasi
 
Back
Top Bottom