Lenin V.I.U
JF-Expert Member
- Mar 28, 2014
- 218
- 62
TCU imekifungia chuo cha IMTU kudahili wanafunzi wapya 2014/2015 hyo ni kutokana na kutotii maagizo waliowapa, miongoni mwa mambo yaliyosababisha kuzuiwa ni pamoja na kutoa ngazi ya cheti bila kufuata utaratibu wa TCU pia kuchukua wanafunz idadi kubwa zaid ya uwezo wake. pia amesema kuwa zoezi hilo halitaathiri wanafunz waliopo pia ametoa miez sita kwa IMTU kurekebisha kasoro hizo.
CHANZO: Mwananchi
TCU yasitisha udahili IMTU
![]()
Kwa ufupi
Uamuzi huo unatokana na chuo hicho kushindwa kutimiza masharti mbalimbali, ikiwamo kutokuwa na wahadhiri wa kutosha na wenye sifa stahiki kama inavyotakiwa na Kanuni ya 15 ya Sheria ya Vyuo Vikuu ya mwaka 2013.
Dar es Salaam
Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), imesitisha udahili wa wanafunzi wapya kwa mwaka wa masomo 2014/15 katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (Imtu) .
Uamuzi huo unatokana na chuo hicho kushindwa kutimiza masharti mbalimbali, ikiwamo kutokuwa na wahadhiri wa kutosha na wenye sifa stahiki kama inavyotakiwa na Kanuni ya 15 ya Sheria ya Vyuo Vikuu ya mwaka 2013.
Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Profesa Mugisha Mgasa imesema baada ya tume kupokea taarifa ya timu iliyotathimini ubora wa chuo hicho kati ya Agosti 25 hadi 28, mwaka huu na wao kufanya ukaguzi, ilibainisha kuwa Imtu imekuwa na mwendelezo wa matukio yasiyoridhisha.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa, TCU imekuwa ikitoa mwongozo kwa chuo hicho kuhusu namna bora ya kutoa elimu ya juu, lakini kimekuwa kikikiuka kutoa viwango bora vya elimu.
Upungufu unaoelezwa ni kudaili wanafunzi wengi zaidi ya uwezo, upungufu wa vifaa pamoja na miundombinu ya kujifunza, kuendesha kozi ngazi ya cheti(UQF) level 6 bila ithibati na kukaidi agizo la tume la kusitisha utoaji wa kozi hiyo.
Imtu pia inadaiwa kufanya taratibu za udahili wa wanafunzi bila kufuata utaratibu wa TCU na uwapo wa wimbi la wahadhiri kuachishwa ama kuacha kazi mara kwa mara, kitendo kinachofanya chuo hicho kuwa na uhaba wa wahadhiri wenye sifa. TCU pia imetoa notisi ya miezi mitatu kwa Imtu kurekebisha upungufu uliopo na ikishindwa kutimiza vigezo hivyo itaweza kufutiwa cheti au hati yake ya ithibati.
Chuo hicho kilihusishwa na viungo vya binadamu vilivyotupwa Dar es Salaam hivi karibuni baada ya kutumika kwa mafunzo.
CHANZO: Mwananchi