TCU wakaribisha maombi mapya.

TCU wakaribisha maombi mapya.

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
18,949
Reaction score
4,646
Tunapenda kuutangazia Umma kuwa tulifunga mfumo wa pamoja wa udahili tarehe 31/08/2016 saa sita usiku ili kuchakata maombi ya waombaji waliofanikiwa kuomba udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Hata hivyo kutokana na wengine kushindwa kufanikiwa kutokana na sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 12 hadi 23 Septemba 2016 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili.
Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza
Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya kwanza
Waombaji wenye vigezo vya Stashahada ambao walishindwa kuomba kutokana na matokeo yao kuchelewa kufika NACTE kwa wakati,
Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka 2016 na matokeo yao yameshatoka,
Waombaji waliofaulu mitihani ya RPL,
Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na uthibitisho toka vyuo vyao vya awali.

Baada ya hapo Tume haitaruhusu tena maombi ili kuruhusu taratibu zingine za kiudahili kuendelea kwa ngazi ya Bodi ya Mikopo na vyuoni.
Asanteni
Imetolewa na
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
02 Septemba 2016
 
Waseme wazi tu huo ufaulu wa D mbili kwa waliomaliza kidato cha sita na GPA ya 3.5 kwa wenye Diploma zimefanya vyuo kukosa wanafunzi sasa wameanza kuhaha.
 
watajuta Ufaulu wa GPA 3.5 kwa diploma na D mbili kwa form six ,wanacheza mdundiko hawa yaani wamelenga kuwachinja wanafunzi wa sayansi
 
Kwa Diploma Gpa ya 3.5 ni shida, bora ingekuwa hata 3.0 hasahasa kwenye fani za sayansi
 
Kwa Diploma Gpa ya 3.5 ni shida, bora ingekuwa hata 3.0 hasahasa kwenye fani za sayansi
Bora wamgesema point 3 kwa form 6 na 3 kwa diploma . au wakaka kwenye 4 ila kwa masomo 3 mwenye dee ndo wapo wengi kitaa
 
Sipati picha vyuo kama tumaini st augustine jordan nelson mandela kama vitapata wanafunzi ata 500
 
Lkn pamoja na kuweka GPA 3.5 lkn still vyuo vimetoa nafasi chache sana kwa diploma kuliko hata wa miaka iliyopita,
 
Back
Top Bottom