TCU na usitishaji udahili baadhi ya vyuo nchini

TCU na usitishaji udahili baadhi ya vyuo nchini

miyanga

Member
Joined
Dec 24, 2015
Posts
38
Reaction score
55
Habari za muda huu wanajamvi nimewaza sana bila kupata majibu ya maswali nayojiuliza kuhusu kuzuia kudahili wanafunzi baadhi ya vyuo kutokana na vigezo mbalimbali kikiwemo Kigezo cha elimu inayotolewa kutokukidhi viwango vinavyohitajika

Swali nalo jiuliza vyuo vilivyositishiwa udahili kisa kukosa hizo sifa na bado kuna wanafunzi wanaoendelea kusoma katika vyuo hivyo Je ni suala la elimu yenye vigezo au? maana kama ni kukosa vigezo wangehamishwa wale waliopo kwani mkiwaacha hapo na elimu inayotolewa haina viwango wataendelea kuipata na kutokuwa na vigezo zaidi

Nadhani kama swala ni vigezo na umeacha wanafunzi hapo kwenye hivyo vyuo waendelee kusoma na unawapa mikopo na huwaamishi basi elimu inayotolewa hapo inavigezo bali kuhusu kuzuia udahili labda kunajambo nyuma yake

Kwa wajuzi wa hizi mambo naomba msaada wa ufaham zaidi je hivi vyuo vinavyo zuiliwa udahili lakini kuna wanafunzi wanaendelea kusoma je sababu ni kukosa vigezo vya utoaji eleimu au kuna sababu nyingine?.
 
Sio kwamba wanafunzi watahamishiwa vyuo vyenye sifa kama ilivyokuwa kwa st Joseph kipindi kile?
 
Back
Top Bottom