TCU:Kanuni zao ziendane na mahitaji

moma2k

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
1,061
1,327
Takwa la walimu wa vyuo vikuu nchini kuwa na GPA ya 3.8 ya undergraduate halina tija. Vinginevyo viwepo vigezo vingine ambavyo ni more superior kuliko kigezo hicho.Mfano: Mtu ana GPA ya undergraduate chini ya hiyo lakini ana PhD, kwanini asipewe fursa ya kufundisha/kuajiliwa kama lecturer? Vyuo vingi havina PhD holders wa kutosha(lecturers,senior llecturers).Matokeo yake undergraduate anafundishwa na undergraduate. Hiyo kanuni ya GPA isipoangaliwa kwa jicho la tatu itasababisha kiwango cha elimu ya vyuo vikuu ishuke. Kuna madokta wengi wa fani mbalimbali lakini hawapati fursa ya kufundisha eti kwasababu hawani GPA inayotakiwa ya undergraduate. Katika viwango vya kimataifa ili chuo kikuu kianzishwe walao nusu ya wahadhiri lazima wawe na PHD. Lakini TZ faculty nzima hakuna mhadhiri mwenye PhD au moja tu. Sheria lazima zipimwe kama zina tija kwa taifa au hapana. Hata hivyo, kwenye uhalisia utaona mtu ana GPA kubwa sana, lakini uwezo wa kujua mambo na kuyafundisha ni zero/sifuri kabisa. PENDEKEZO: 1.Kadiri ya utafiti wangu kwa masilahi mapana kwa taifa kigezo hicho kifutwe kabisa au viwepo vigezo vingine vyenye tija ambavyo vinapimwa kwa performance,competance and capability to deliver. 2.Msomi yeyote mwenye kiwango cha PhD aruhusiwe kuwa MHADHIRI wa chuo kikuu. Hii itasaidia kuongeza quality of higher learning products. Maana sasa vyuo vikuu vingi havina hadhi ya kuwa vyuo vikuu. No research no what. Ni copy and paste only. Ni kama secondary tu.
 
Back
Top Bottom