TCRA Yatakiwa Kuchukua Hatua Madhubuti Kudhibiti Utapeli wa Kielektroniki Kupitia Ujumbe wa Simu

TCRA Yatakiwa Kuchukua Hatua Madhubuti Kudhibiti Utapeli wa Kielektroniki Kupitia Ujumbe wa Simu

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Ni Jumapili juzi nikiwa zangu mitaa ya Arusha natoka zangu kumshukuru Mungu basi nikaona ni vyema nijiandae kutoka out kidogo nikatafuta sehemu kuna wakala wa huduma za kifedha. Nikauliza kama naweza kutoa pesa na alinikubalia kuwa nitoe huku akinipa na namba ya kutolea.
images - 2025-04-14T222505.882.jpeg

Dakika kama tano alikuja Bibi Mmoja akiwa anahitaji kutuma pesa kwa mjukuu wake hivyo alimuuliza mtoa huduma kuwa anaweza kutuma pesa kwa mjukuu wake. Yule bibi alimpatia namba mtoa huduma na kumpa laki 8, mtoa huduma alifanya kutuma ule muamala akiwa anajua kuwa namba ni sahihi.
images - 2025-04-14T222350.447.jpeg

Lakini ajabu ni kuwa yule Bibi alipomtafuta kijana wake alidai kuwa hajapokea pesa yoyote na hiyo namba sio yake. Tulimsaidia kutazama namba tukakutana na tapeli mmoja aliyemtumia ujumbe wa TUMA KWENYE NAMBA HII. Bibi wa watu presha ilipanda pale pale ila tulimsaidia kumpeleka kituo cha afya.
images - 2025-04-14T222332.320.jpeg

Lakini je, ni kwa nini haya yanaendelea kutokea? Na je, kuna njia ya kukomesha kabisa?

TCRA – Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania – ina nafasi ya kipekee sana ya kuwa ngome kuu dhidi ya utapeli huu. Kwa kutumia teknolojia zake za hali ya juu, TCRA inaweza kuanzisha mfumo wa kitaifa unaoweza kuchambua, kugundua, na kuzuia ujumbe wa ulaghai hata kabla haujamfikia mtumiaji.
images - 2025-04-14T222246.006.jpeg

Nina imani kuwa mfumo huu unaweza kuunganishwa moja kwa moja na mitandao ya simu ili kuweza kutambua namba zinazotumiwa mara kwa mara kwa utapeli na kuzizuia moja kwa moja.
images - 2025-04-14T222214.724.jpeg

Mfumo huo unaweza pia kuwa na uwezo wa kutambua ujumbe wenye lugha za hadaa kama vile: “Mimi mwenye nyumba tafadhali tuma kodi leo”, au “Mama anaumwa sana– nitumie salio.” Kwa kutumia teknolojia kama vile (AI), Internet of Things pamoja na (Big Data), ujumbe wa namna hii unaweza kuchujwa, kuchunguzwa, na kufutwa kabla haujawafikia walengwa.
images - 2025-04-14T222158.190.jpeg

Shirikianeni na mamlaka za sheria kuweka sheria kali sana kwa wale ambao watakutwa na kesi hizi. Vifungo virefu visivyopungua miaka 50 kwa hakika itakomesha kabsa huu upuuzi ambao unawatesa sana watu mitaani.

TCRA NI MALI YA WATANZANIA WOTE, SAIDIENI WANANCHI.
 
Back
Top Bottom