TCRA wako serious kweli?

Mkiu Kwetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2017
Posts
261
Reaction score
280
Wakuu kwanza niwape pole kwa jitihada zenu za Ujenzi wa Taifa.

Bila kuwachosha, naenda moja kwa moja kwenye mada.

Nimeweka kichwa cha habari katika hali ya swali ili niweze kupata maoni kulingana na uelewa wenu.

Leo nilikuwa napita pita mitaa ya fb, nikaingia kwenye account moja inaitwa "Angel John's"

Kwa kweli niliyoyaona humo in aibu tupu, yaani hilo no gulio la biashara ya ngono, tena lipo wazi kabisa, na cha kushangaza kuna mpaka kiingilio ili uunganishwe na Malaya unayemtaka.

Mabinti wadogo wadogo, wazuriii, wanajitangaza uchi kabisa bila hata aibu wanaonyesha maumbile yao, Kweli Mwenyezi Mungu ameumba bwana, lakini in kwa ajili hiyo?

Nimejiuliza maswali mengi sana ambayo mengine nimekosa majibu;
1. Je hawa mabinti hawana wazazi? hata ndugu tu katika jamii kwamba hata waone haya kuonyesha tupu zao mitandaoni?

2. Je, in ushamba was matumizi ya mitandao?

3. Wameshindwa kabisa kufanya shughuli nyingine yoyote halali yenye heshima katika jamii?

4. TCRA hawaoni mmomonyoko huo was maadili ya kitanzania yanavyotokea,? Na hatua gani wanachukua kunusuru jamii kuharibika?

5. Jeshi la polisi linafanya doria mitandaoni, je mtaa huo hawajapita? Au wanapitia mitaa ya kina Giggy Money tu?

Kweli nimefadhaishwa sana na hamu hiyo, naomba mwenye ufahamu zaidi anijuze tafadhali.

Naomba kuwasilisha.
 
TCRA wapo serious kwenye mambo mengine, sasa hivi kipaumbele ni uchochezi, jaribu kufungua account yoyote halafu uchochee kidogo, watakudaka kama mwewe anavyovidaka vifaranga😀
 
Usikute umeweka tangazo.
Hata hivyo TCRA hawama uwezo wa kuzuia hiyo account, wasiliana na FB wenyewe.
 
Hilo ni tatizo LA dunia nzima.
Tumuombe Mungu atusaidie lakini tuba wajibu wa kuwalea na kuwa wawazi kwa watoto wetu.
Lakini mtoa mada umewapromote hapo ulio wataja
Lengo sio hilo, my take is, ziko acc nyingi za hivyo lakini hakuna anayechukuwa hatua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…