TCRA usumbufu huu wa makampuni ya simu utaisha lini?

kipindupindu

JF-Expert Member
Dec 16, 2010
1,053
170
Kwa wateja wa voda mtakubaliana nami kuwa kuna wimbi la sms kutoka kwa hawa service provider wetu,sms hizi ni za kihuni na zinaleta usumbufu mno,unaweza ukahairisha kwenda chooni ukakimbilia mlio wa simu unaoashiria sms ukitegemea ni message muhimu imeingia kumbe looo!
Ukifungua unakutana na haya :

"umebahatika!
Katika mchujo namba 075****** yaweza kushinda usiku huu tsh 3000000 taslimu na vodacom!Tuma jina lako kwenda 15544 haraka!550tsh/sms "

hapo utaamua kuuchuna basi watakurushia hii hapa:

"una neema!usichukulie ujumbe huu ki mzaha tuma jina lako haraka kwenda 15544 na waweza shinda Tsh 3,000,000 taslimu ya vodacom usiku huu!550 Tsh/sms "

ukiwa ngangari zaidi hawakuachi wanakupiga na hii: (wakuu hii imenichekesha kidogo haswa hiyo sehemu ya kwanza)

"WASTAHILI SIFA! tulijaribu kuwasiliana na wewe na hukujibu!muda ni sasa tuma jina lako kwenda 15544 na waweza shinda leo tsh 3M taslimu na vodacom!550 Tsh/SMS"

Sijui sasahivi watakuja na gia ipi?

My take:huu ni usumbufu kwa wateja halafu kwa nini mnalazimisha watu kucheza bahati nasibu?
Hivi kama mh mkuu wa kaya/waziri wa mawasiliano ana line ya voda naye hutumiwa hizi sms? TCRA MKO WAPI?au mnaiwinda Jf?

Nawasilisha...
 
kwa hilo hata mimi nakereka sana imefika wakati naona kama huu mtindo ni wizi mtupu kwa makampuni haya ya cm kwanza wanatusumbua kwa sms kibao zisizo hata na umuhimu kwetu inshort wanatuboha!
 
hii ni issue ambayo inabidi iangaliwe kwa pamoja na TCRA pamoja na bodi ya bahati nasibu!
 
Back
Top Bottom