TCRA tunusuru kwa hili ili tulinde maadili ya watoto wetu

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,575
8,595
Naanza kuwaomba TCRA kwakufahamu ndiyo chombo pekee kinaweza kusaidia hili nitakalolisema kwakuwa ndio wenye dhamana.

Niombe niseme hivi...
Kuna matangazo yanayotolewa katika Radio na Television yanakuwa na ukakasi hata kuyasikia hasa pale unapokuwa umekaa na watoto wako au hata mamayako,baba yako. Nitatolea mfano tangazo moja.

SIGWA HERBAL CLINIC wanatangazo linaukakasi sana utasikia wakisema kutokwa na uchafu katika via vya uzazi!Mwanamke hutokwa na harufu mbaya hii ni dalili..........so and so!Kwa kweli hili tangazo katika Radio ni baya pia linadhalilisha mwanamke katika jamii pia kwanini hizi Herbal Clinic zote kwanini watoe wajii wa ugonjwa katika matangazo?

Hivyo niwaombe TCRA kupiga marufuku matangazo ya namna hii pia kulifungia tangazo la SIGWA HERBAL CLINIC.

Natanguliza shukrani za awali.
 
maradhi yetu ndio mtaji kwao. kufungiwa kwa kukiuka taratibu na kanuni za uendeshaji kuko sawa, je suluhisho la tiba kwa sisi wateja serikali na mamlaka zilizohusika kupiga kufuri zimejipangaje? maana hizi kliniki lau zilikuwa zinanya mobile services. utasikia wana matawi kanda mbalimbali na kuna baadhi wamenasa sauti za wateja wakishuhudia tiba zao kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. je hatutaambiwa kuendelea na tiba Muhimbili, Apollo, S. Africa n.k!!!
 
Back
Top Bottom