Hili la TCRA, huu ni mwendelezo wa kuminya uhuru wa habari, uwazi na uwajibikaji wa watanzania

Apr 23, 2012
76
71
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka Michuzi TV, AYO TV na Global TV kusitisha huduma zao za TV mtandaoni hadi hapo kanuni za usajili rasmi ambazo mamlaka hiyo imesema inaandaa kwa huduma hizo zitapokuwa tayari.

#My_Take
..., niendelee kusema ukweli tu.., hii kitu imeniumiza sana (mimi siyo kati ya hao waliofungiwa) lakini nimeguswa na namna mamlaka hii inavyoendeshwa.., unakwenda kuzuia huduma isitolewe wakati hizo kanuni hata kutungwa bado na hazipo..,

.., TCRA wanazuia [online TV] zisifanye kazi kwa sababu zinafanya kazi bila utaratibu, wakati hata huo-utaratibu wa usajili hawajauanzisha. Wanasema [hawa watoa huduma] wasitishe kufanya kazi kusubiri utaratibu wa usajili na usimamizi ambao utaanzishwa na TCRA...,

.., ninyi TCRA, mmeshindwa nini kuweka hizo kanuni, kisha ndiyo "mzime" au "mkataze" leseni kwa wale ambao watakuwa hawana leseni hizo!? Kuna baadhi ya watoa huduma, waio tayari hata leo kukamilisha taratibu za usajili kama zingekuwepo.., na kwa sababu bado [hizo taratibu hazipo] na hata kukamilika bado, kwanini "msitoe" muda zaidi chini ya uangalizi wakati [wakati] watoa huduma wanasubiria kanuni hizo mpya?

.., hizi huduma za habari za video mitandaoni [online Television] zimekuwa msaada mkubwa wa habari kwa haraka sana, tunapata [sisi wananchi] habari kwa haraka sana, hata zile habari ambazo hazipewi kipaumbele kwenye vituo vya televisheni, hizi (online Tv),

.., mnawaeleza hawa watoa huduma za haraka za habari waache kutoa huduma zao, unawaambia wasitishe kurusha matangazo kwa sababu hawafuati utaratibu, wakati utaratibu wenyewe haupo, haujaanzishwa.., utaratibu huo utaanzishwa lini? Mmetoa deadline ya kutengeneza "utaratibu huo"!? [kwanini msiwatake] waendelee na shughuli zao, hadi hapo [ninyi TCRA] mtakapokamilisha huo utaratibu wenu? Kisha ndiyo" mtake kwa mbwembwe "sasa waanze kufuata utaratibu.

Sheria ya usimamizi wa [online TV na radio] nchini kwetu haipo...., ni kwa nini usiruhusu waendelee [hawa watoa huduma] kutoa huduma zao hadi hapo hiyo sheria itakapoanza kutumika rasmi? (vinginevyo), Mtueleze sasa hili zuio ni kwa ajili ya baadhi ya matangazo ya bunge, kwa sababu vipindi vya bunge vingi, tunavipata kupitia [online television] hizo.., [lasivyo] mtueleze sisi wateja wao, huduma zao zina athari ipi kuendelea kuwa hewani wakati wakisubiri hizo [regulations] zenu..?

Agizo hilo ni kwa ajili ya Bunge. Matangazo ya Bunge yamesitishwa live. Hizi online TV ndio zilikuwa zinasaidia kwa kuchukua vipande muhimu na kuweka online. Kupitia Facebook page Jamii Forums hurusha live Bunge..., Wenye kumiliki simu tanashati [smartphone] kamwe hawapitwi na baadhi ya vipindi vya Bunge kwa sasa. Online TV zinafanya kazi hiyo vyema sana, haswa Global Tv, AYO Tv na hata Mwananchi online..,

.., Uamuzi huu wa kupiga marufuku [online TV] ni kwa ajili ya kuondoa kabisa matangazo ya Bunge, ambayo mara nyingi wananchi wamekuwa wakipata kupitia Televisheni hizo za mitandaoni... Leo lengo lenu liko wazi tu, wote tunaamini kwamba, [lengo lenu] ni kuwafanya wananchi waendelee kuwa "vipofu wasiokuwa na utimamu" na kamwe [wasijue] kile ambacho kinaendelea katika bunge lao...,wala hili suala halihitaji akili kubwa kugundua hili kwa haraka...

.., hivi mnakwenda ninyi [TCRA] vipi kulipa gharama za mikataba [baina ya] kampuni za kibiashara na watoa huduma hizo za [online Tv], ambayo hawa jamaa wameingia na kampuni hizo? Hivi mnajua athari yake? Vipi kama kampuni hizo zikitaka kulipwa fidia kwa namna yoyote ile na hawa watoa huduma hizo!? Mtawapa msaada wa kisheria au malipo ya fidia hizo!? Kwamba (mmeshindwa) kutumia busara, hawa watoa huduma waendelee na shughuli zao, wakati ninyi [TCRA] mkiendelea na huo utaratibu wa kuleta hizo kanuni na taratibu zenu!

.., Sijui mnataka Millard Ayo, Issa Michuzi na wengine waendelee kuajiriwa tu...., yaani vijana wa watu wamejipiga, wamefanya kazi bidii zote, wamenunua vifaa [kwa gharama], wamebuni mambo makubwa, wameamua kujiajiri na pia kutoa ajira kwa vijana wengine, leo mnakuja kuwataka watoto hawa wa kitanzania [labda ni maskini hapo awali], leo hawa wabunifu warudi nyuma na kusubiri sijui sheria, sijui kanuni, sijui utaratibu..., mambo ya ajabu sana..,

.., wakati huo mnasema watu wajiajiri, wafanye kazi..., kwa hiyo wale waandishi wa habari na watangazaji wa Millard Ayo TV na Mivhuzi Tv etc, wakajiajiri wao wapi tena..., (kesho mtaanza tena kuwazoemea kwamba hawana kazi, na kwamba hawataki kufanya kazi, wakati ajira zao mmesitisha ninyi wenyewe kwa matakwa yenu binafsi).., kweli hii ni nchi ya VI - wonder!

Martin Maranja Masese (MMM)
 
Mkuu nashukuru kwa kuleta hichi kitu hapa binafsi niliwaza sababu kubwa ni hizi clip za bunge tunazo access
 
Back
Top Bottom