TCRA Msiache kuzima hizi makampuni za simu, voda ikiwemo

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,740
21,186
Twende moja kwa moja kwa mada.

Umemuomba mtu pesa ili ununue dawa kwa ajili ya mgonjwa uliyemuacha hospitali ukiwa njiani unasikia mlio wa meseji, unasogea pembeni kwa tashwishwi kuwa jamaa yako kakusapoti.

Au unadhania ni taarifa kutoka hospitali ulipomuacha mgonjwa kuwepo kwa mabadiriko mara unakutana na upuuzi, meseji ya ovyo kabisa ya TANGAZO, moyo unakata nguvu na kuanza kuikasirikia simu.

TCRA nyie ndiyo washika dau wakubwa, wakati huu mnapozima line za wasiosajiliwa na hawa muwazimie hizi kitu hazina faida kwangu.

Shame on them.
 
Huwa inakera sana, kuna siku nimetingwa nasubir hela iingie mara naona limesej la PESA NI M-PESA, na kila siku lazima wanitumie hili li sms tena liko vilevile yan inakera sana aisee
 
Mimi nime block wote haoo
Mkuu tupe njia uliyotumia na hazikufikii hizo sms, maana nilijaribu kublock ila zinaingia kimya kimya na pale juu unakiona kibahasha kikikukupa taarifa.
 
Guys kama mnatumia smartphone za kisasa mbona mnaweza kublock hizo messages. Pakua app ya message ya google then click hiyo message kisha bofya block & report spam.. kwishaaaa.
 
Block meseji zao kwa app ya google message.
20200125_233535.jpeg

20200125_233614.jpeg

20200125_233711.jpeg
 
Mkuu tupe njia uliyotumia na hazikufikii hizo sms, maana nilijaribu kublock ila zinaingia kimya kimya na pale juu unakiona kibahasha kikikukupa taarifa.
Mimi nmeblock zote za tatu mzuka za pesa Ni mpesa na cjui zile za kubet.... Zinaingia kwa cm yangu ila bila notification yoyote na Wala haziendi inbox....
Kwenye settings za cm yangu nlipoenda Kuna mahali ikanionyesha ivyo... Hata pale kwenye sms box Kuna mahali pameandikwa general settings Napo pia ipo iyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom