mkalimani4
Member
- Nov 30, 2016
- 26
- 29
Napenda kwanza niwape hongera kwa kazi nzuri mnayoifanya hasa ya kuwapa habari wananchi kuhusu haki zao za kupata habari. Nakumbuka mwaka juzi mlitangaza kuwa Channel za ITV, EATV,TBC, CLOUDS n.k zinatakiwa kuonyeshwa bure na King'amuzi cha Continental hata kama mteja hajajiunga na kifurushi chao.
Hivi sasa agizo lenu limewekwa kapuni na sasa wameachia channel tatu tu;- Star tv, Tbc na Tanzania Safari.
Mkuu wa Tcra wachunguze vijana wako inawezekana wamepewa mlungula na kampuni hilo ili wavae miwani ya mbao kwa kutoona jinsi wananchi wanavyonyimwa haki ya kupata habari.
Kama leseni yao walibadilisha ni vyema jamii ikafahamishwa kuliko kuwa na ukimya wa namna hii.
Pia nimebaini hata King'amuzi cha Zuku kinalipisha hata channel ya Tbc kama kifurushi kikiisha na yenyewe inasitishwa.
Natumaini mtafanyia kazi suala hili.