TCRA Mko wapi Jamani? Voda wanazidi kutufanya Maskini!

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,905
25,745
Hivi TCRa mnafanya nini?
Mnataka mpaka turudi kijijini mbaki mafisadi wenyewe ndio mtakaposhtuka kua tuna maskinishwa na Vodacom?
Wameniunganisha kwenye promosheni yao inaitwaje sijui but kila siku wananikata Tshs 550/=,
Nimejaribu kutuma maneno mbalimbali ya kujitoa kama vile "ondoa", "cancell", "toka" n.k. na kila nikituma hua wananiahidi kutonitumia tena meseji zao lakini bado wananendelea kunitumia,
Sielewi kama hii promosheni ni Lazima ama vipi?
Mtu unaweza kuweka ka-alfu kako ukiwa ushabajeti, soon Tshs 550/=inaliwa, huu ni wizi uliohalalishwa huu.
Nakumbuka maneno ya Mbunge wangu mmoja kua Mitaani tunaishi na wahalifu waliohalalishwa wengi tu.
 

G. Activist

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
482
125
Pole sana Bro... ni sms za nn hizo bro ulizojiunga nazo?? Inaonekana mwanzoni ulizifurahia kweli hata hukuona 550 ni nyingi!!! Lakini sio waungwana kabisa!!! IT wao cjui wanafanya nn...!!!
 

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,905
25,745
Kila siku wananikata Tshs 550/= kwa kunitumia meseji eti "Sishikiki", maana yake nini hii?
Sishikiki kivipi?
Na sishikiki na nani na kwanini? Wao wanashikika?
Anaeshikika yukoje?
Na nashikikia wapi?
Sio kutukanana huku jamani?!!
 

Butola

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
2,290
748
Tatizo halitatuliwi kwa kulikimbia,
Wacha kukariri wewe!!

Hili ndilo tatizo letu..

Yaani Voda wamekukera, wamekuibia, wewe unanung'unika tu kwenye mtandao badala ya kuwafuata kupeleka malalamiko yako rasmi au kuwagharimu kwa kuacha kutumia huduma zao?

Ndugu yangu, mtandao sio baba yako, wakitoa huduma mbovu,either ulalamike au uachane nao kwa kuhamia mtandao mwingine utakaokupa huduma bora zaidi, ndio maana ya kuwepo ushindani wa huduma hizi, kama tukiendelea kuwa watiifu hivi kwa makampuni haya katika wakati huu wa soko huria, tutarajie huduma mbovu na kandamizi zaidi siku chache zijazo, chukua hatua..

HII NIMEITOA KWENYE MTANDAO WA TCRA>> http://www.tcra.go.tz/customer/complaints/Mwongozo_wa_mamalamiko.pdf

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inatoa mwongozo huu wa kushughulikia
malalamiko ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano kwa mujibu wa Kifungu cha
40 Sehemu ya VIII ya Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka
2003.

Ni muhimu kuzingatia kuwa Mwongozo huu unatumika kwa mujibu
wamalalamiko ya mteja wa bidhaa na huduma za posta na mawasiliano ya
kielektroni au huduma zinazohusiana na usambazaji wa bidhaa au huduma za
posta na mawasiliano ya kielektroni isipokuwa kwa malalamiko yanayohusiana
na mambo ya utangazaji. Madai hayo lazima kwanza yawasilishwe kwa mtoa
huduma na mlalamikaji na mtoa huduma lazima apewe kiasi cha siku thelathini
(30) kulitatua tatizo hilo kabla ya kulifikisha TCRA. TCRA haitakubali
uwasilishaji wa malalamiko isipokuwa pale ambapo mlalamikaji hakuridhishwa
na utatuzi uliofanywa na mtoa huduma. Hata hivyo, iwapo malalamiko
yatapelekwa TCRA wakati wa tukio la kwanza, yatarudishwa kwa mtoa huduma
anayehusika.
 

Washawasha

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
16,219
12,265
watumie sms kuwa unaachana nao kwasababu hiyo uliyoieleza halafu USIUTUMIE TENA MTANDAO HUO.
 

Mike 1234

JF-Expert Member
Feb 23, 2009
1,633
154
tatizo siyo voda,bali ni wewe mwenyewe kabla hujajibu chochote soma masharti yake kwanza,huu mchezo uko mitandao yote na si voda tu,ila pole mi zain walinitafuna hasa
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,548
6,671
nyie msiwatetetee tatizo sio kuama tatizo ni kuibiwa, kuna mtu anadakia anasema si uamie airtel? je? na wao wakifanya hivyo, wewe utakuwa bwana kuhama?
 

juniorfeb18

Member
Apr 12, 2011
36
14
nilifikiri ni mimi peke yangu,nimejitoa mara nyingi mno,bado nakatwa,nimepiga costomer care,hawataki kupokea,nimeamua kuweka salio la mia tano,wananitumia sms insufficient fund!!yaani hawa watu nimweziiiiiiiii
 

LebronWade

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,615
1,501
tatizo siyo voda,bali ni wewe mwenyewe kabla hujajibu chochote soma masharti yake kwanza,huu mchezo uko mitandao yote na si voda tu,ila pole mi zain walinitafuna hasa

Mkuu Mike,heshima yako....tunachotaka hapa sio muongozo wa TCRA ambao karibu Watanzania zaidi ya 40milioni hawana access nao,achilia mbali watanzania wasiojua kusoma...tunachotaka hapa ni kwamba asietaka aweze ku-opt out bila wizi wa kuendelea kumtumia mtu huyo msg na kumkata vihela vyake vya jasho....hapa ni normal practice na uungwana tu kwamba kama sitaki basi mnitoe msile hela yangu,ila haya mapumbavu yanaendelea kukata tu...majambazi haya majitu.
 

Butola

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
2,290
748
Mkuu Mike,heshima yako....tunachotaka hapa sio muongozo wa TCRA ambao karibu Watanzania zaidi ya 40milioni hawana access nao,achilia mbali watanzania wasiojua kusoma...tunachotaka hapa ni kwamba asietaka aweze ku-opt out bila wizi wa kuendelea kumtumia mtu huyo msg na kumkata vihela vyake vya jasho....hapa ni normal practice na uungwana tu kwamba kama sitaki basi mnitoe msile hela yangu,ila haya mapumbavu yanaendelea kukata tu...majambazi haya majitu.

Mkuu hatupo kwenye ulimwengu wa Azimio la Arusha, huu ni wakati wa Upepari ambapo pesa ni zaidi ya utu, Wawekezaji hawajaja hapa nchini kueneza UTU bali ni KUTAFUTA PESA.

Hakuna njia ya mkato kwenye kudai haki, ni either UCHUKE HATUA KWA KUFUATA TARATIBU ZA KISHERIA, UGOMEE HUDUMA ZAO AU UKAE KIMYA MILELE, uchaguzi ni wako...
 

vivian

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
1,749
998
ha ha ha ha ha ha ha.. Pesa za kujaza Helcopter mafuta kule Igunga.

Kuna siku nimetumiwa message eti wimbo wako ulioomba kwa anayekupigia simu umekubalika Gharama Tshs. 500. Shortly nikatumiwa wimbo wa hata sikumbuki vizuri uliomba umekubaliwa- umakatwa 210 kwa huduma hii.

I was really pissed off. Nachukia sana ninapompigia mtu simu halafu naimbiwa minyimbo ya ajabu ajabu wakati mimi nimeshajichokea zangu nataka kupumzisha akili.

VODA COM is the most expensive in Tanzania Currently.

With 2,500 you get 400mb internet bandle from zain which you can use for a month. to get 400mb from Voda you have to pat with Tshs. 16,000.

While 10,000 you can get 500mb internet bandle from Zantel- iko fast sana even more than Voda

Nilsha achana na voda katika matumizi ya kila siku, watanipata kwenye M-Pesa tu!!!!
 

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,201
1,331
Mkuu wafatilie na kama inawezekana pitia kwa mwanasheria mmoja na awaandikie barua ya madai kwamba ni kiasi gani umepoteza (ingawa kwanza soma small prints uone kama hazikufungi...)

Wakuu issue sio kuhama karne hii karibia kila mtu ana simu za mitandao yote; hivi ukihama mtandao mmoja wale associates wako ambao unaongea nao wakiacha kukupigia ni hasara ya nani..?; issue ni kuwabana watu au kampuni yoyote inapokiuka sheria.., tena na kudai ile hasara yote iliyotokea..., am sure kwa kuogopa bad publicity watakurudishia pesa..., alafu hakikisha kwamba ni voda ndio wanaoendesha hio kamali sababu uenda ni third part company...., Jipange; Fahamu Haki Yako.., Alafu Attack...!!!
 

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,856
1,101
Kila siku wananikata Tshs 550/= kwa kunitumia meseji eti "Sishikiki", maana yake nini hii?
Sishikiki kivipi?
Na sishikiki na nani na kwanini? Wao wanashikika?
Anaeshikika yukoje?
Na nashikikia wapi?
Sio kutukanana huku jamani?!!

aah bh hushikiki mkuu!
 

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,729
387
Tatizo wanaposema "vigezo na masharti kuzingatiwa" huwa hawasemi hayo masharti na vigezo ni vipi
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,538
5,646
Kila siku wananikata Tshs 550/= kwa kunitumia meseji eti "Sishikiki", maana yake nini hii?
Sishikiki kivipi?
Na sishikiki na nani na kwanini? Wao wanashikika?
Anaeshikika yukoje?
Na nashikikia wapi?
Sio kutukanana huku jamani?!!

umenifurahisha. Punguza hasira.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom