TCRA kufungia laini za simu milioni 15

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
sim cards.jpg

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema itazima jumla ya laini za simu milioni 15 katika awamu ya tatu.

Fredrick Ntobi, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma TCRA amesema wananchi wanapaswa kutambua kuwa zoezi la kuzima laini ambazo hazijasajiliwa kwa mfumo wa alama za vidole halijasitishwa wala kuahirishwa na badala yake zitazimwa kwa awamu tofauti, lengo likiwa ni kupunguza usumbufu kwa wananchi wanaoendelea na zoezi la kusajili laini zao.

Aidha amesema awamu ya kwanza tayari ilikamilika, huku awamu ya pili ikiwa imekamilika tarehe 26 Januari, na sasa wanaelekea kutekeleza awamu ya tatu.

Hata hivyo wasajili katika baadhi ya vituo wameeleza kuwa mwitikio wa wananchi kusajili laini umepungua tangu zoezi rasmi la uzimaji lilipoanza, na kwamba wachache hao wanaojitokeza katika vituo hivyo ni wale waliofungiwa laini zao.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom