Jumakidogo
R I P
- Jul 16, 2009
- 1,851
- 417
Imefika wakati sasa kwa mamlaka zinazohusika kusikiliza malalamiko ya wananchi ili ufumbuzi upatikane. Sasa hivi mitaani, kwenye mitandao ya jamii watu wanapiga kelele kuhusu wizi wa kampuni hii ya simu inayoitwa TIGO. Siamini kama mamlaka husika mfano TCRA hawalijui hili, kwani bila shaka miongoni mwao wapo wanaotumia mtandao huu. Wabunge wetu najua nao miongoni mwao wapo wanaotumia mtandao huu. Hata uongozi wa juu wa kampuni hiyo siamini kama hawajui kinachofanyika katika kampuni yao. Huduma zao zimekuwa mbovu na gharama kubwa. Sioni sababu ya kukata pesa mtu unapiga simu, unayempigia kama simu yake haipatikani, ukichelewa kidogo kuondoka hewani. Wanakata salio. Mbaya zaidi kama una tatizo ukitaka kuwasiliana na mshauri au huduma kwa wateja. Simu yao unalipia hata kama tatizo lililokupata limesababishwa na wao wenyewe. Kibaya zaidi simu yao ukipiga haipokelewi kamwe. Hebu kwa uchunguzi wa awali kama kuna muhusika kutoka TCRA hapa jamvini apige namba hii ya huduma kwa wateja TIGO aone kama itapokelewa: 0713800800. Tunaomba serikali na mamlaka zinazohusika zitusaidie wananchi. Ufumbuzi si kuhama kampuni, ni kutatua tatizo.
Wateja wa Tigo fanyeni petition (kusanyaneni saini za wateja walioudhika) halafu muwaandikie na nakala mpeleke na TCRA, WMU, BoT (kwa ajili ya Tigo Pesa) na WF, pia nakala kwa consumer body iliopo chini ya WMU, na wengineo wanaohusika. Kuendelea kulalamika humu jamvini hakuta badili chochote
Hilo kweli, mimi situmii TiGo kupiga simu zangu, natumia modem yao kwa internet tuu, lakini juzi ndio nimeamini kuwa 1) wizi na 2) waongo. Natumia kifushi cha max na bahati nzuri kimekwisha kabla ya mwezi, ingawa wao wanasisitiza kuwa hata 1.5gb wanazokupa zikiisha utaendelea kutumia modem. Cha kushngaza ni kuwa kweli, unaingia kwenye internet lakini site zote hupati, wantazama trend yako tu, na wanakuwachia sites kama za email na JF pekee. Hupati hata wikipedia, hupati chochote ukitafuta kutokea google
Huu ni wizi wa waziwazi. Si wangesema tu, zikiisha nunuwa kifurushi kingine, kuliko kuwacha tunahangaika kutafuta ushauri, labda PIPA, labda mtandao mbovu, labda websites zimefungwa, yaani wanachofanya ni kitu kibaya sana tena sana, Na nikijia mjini nanunua modem nyingine na kadi yao naivunjavunja na kuitupilia mbali, naomba na wengine wafanye hivyo. Dawa yao haya makampuni ni kuwasusia tu.
Hilo kweli, mimi situmii TiGo kupiga simu zangu, natumia modem yao kwa internet tuu, lakini juzi ndio nimeamini kuwa 1) wizi na 2) waongo. Natumia kifushi cha max na bahati nzuri kimekwisha kabla ya mwezi, ingawa wao wanasisitiza kuwa hata 1.5gb wanazokupa zikiisha utaendelea kutumia modem. Cha kushngaza ni kuwa kweli, unaingia kwenye internet lakini site zote hupati, wantazama trend yako tu, na wanakuwachia sites kama za email na JF pekee. Hupati hata wikipedia, hupati chochote ukitafuta kutokea google.
Huu ni wizi wa waziwazi. Si wangesema tu, zikiisha nunuwa kifurushi kingine, kuliko kuwacha tunahangaika kutafuta ushauri, labda PIPA, labda mtandao mbovu, labda websites zimefungwa, yaani wanachofanya ni kitu kibaya sana tena sana, Na nikijia mjini nanunua modem nyingine na kadi yao naivunjavunja na kuitupilia mbali, naomba na wengine wafanye hivyo. Dawa yao haya makampuni ni kuwasusia tu.
Dear Customer,
Thank you for your candid feedback. It is difficult for us to assist you without further details such as your number and time of occurrence of problem. Please include such information whenever you convey your concerns.
Please note that every operator charges for calls directed to customer care to avoid playful calls and ensure only customers who have issues are served.
We do have channels which you can utilize to raise your concerns free of charge. We have call centers and various locations and also a Facebook page where we provide the best and timely customer care services.
Whenever you have any concern, query or suggestion, please convey it to us through our Customer Care tab on our Facebook page on www.facebook.com/TigoTanzania.
Tigo