TCRA, kampuni ya mawasiliano inayoitwa TIGO inatuibia Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TCRA, kampuni ya mawasiliano inayoitwa TIGO inatuibia Watanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Feb 5, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Imefika wakati sasa kwa mamlaka zinazohusika kusikiliza malalamiko ya wananchi ili ufumbuzi upatikane. Sasa hivi mitaani, kwenye mitandao ya jamii watu wanapiga kelele kuhusu wizi wa kampuni hii ya simu inayoitwa TIGO. Siamini kama mamlaka husika mfano TCRA hawalijui hili, kwani bila shaka miongoni mwao wapo wanaotumia mtandao huu. Wabunge wetu najua nao miongoni mwao wapo wanaotumia mtandao huu. Hata uongozi wa juu wa kampuni hiyo siamini kama hawajui kinachofanyika katika kampuni yao. Huduma zao zimekuwa mbovu na gharama kubwa. Sioni sababu ya kukata pesa mtu unapiga simu, unayempigia kama simu yake haipatikani, ukichelewa kidogo kuondoka hewani. Wanakata salio. Mbaya zaidi kama una tatizo ukitaka kuwasiliana na mshauri au huduma kwa wateja. Simu yao unalipia hata kama tatizo lililokupata limesababishwa na wao wenyewe. Kibaya zaidi simu yao ukipiga haipokelewi kamwe. Hebu kwa uchunguzi wa awali kama kuna muhusika kutoka TCRA hapa jamvini apige namba hii ya huduma kwa wateja TIGO aone kama itapokelewa: 0713800800. Tunaomba serikali na mamlaka zinazohusika zitusaidie wananchi. Ufumbuzi si kuhama kampuni, ni kutatua tatizo.
   
 2. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Tulishaama zamani kaka, hata kumpuguzia mwenzio wanakata ela! hawa jamaa ni wezi wa kutupwa ni zaidi ya majambazi, line yao naitumia kwa kupokelea tu, hata airtel ni majambazi pia, unaweza kutumia dk 2 lakni wakakukata zaidi ya sh. 360, wakati wanasema wanatoza sh. 1 kwa sekunde! mm nimeamua kupokea tu wala sipigi siku hizi
   
 3. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mkuu hapo umenena nliwahi pata tatizo la transaction tigo pesa nkiwa Arusha walahi nlipiga simi namba zifuatazo lakini hazikupokelewa..100,150,0713800800...i was about to loose my money ..Mungu si Athumani jamaa mmoja rafiki yangu anfanya kazi tigo ndo aliyenisaidia....Customer care ya Tigo hovyo sana.
   
 4. M

  Mbuli Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kuna mitandao mingi sana kaka, halafu hakuna ulaqzima wa kukaa Tigo. Kama unaona ni wezi asi hama haraka sana kimya kimya... Ingekuwa Tanesco sawa. Lkn Tigo au CCM we unahama bila hata kumfahamisha yyte
   
 5. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Wateja wa Tigo fanyeni petition (kusanyaneni saini za wateja walioudhika) halafu muwaandikie na nakala mpeleke na TCRA, WMU, BoT (kwa ajili ya Tigo Pesa) na WF, pia nakala kwa consumer body iliopo chini ya WMU, na wengineo wanaohusika. Kuendelea kulalamika humu jamvini hakuta badili chochote
   
 6. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  TCRA wao wamelala tu nafikiri wakishatoa licence wanarudi kitandani kulala bila kumlinda Mtanzania. Ujue ni ujinga sana TCRA wanafanya hasa katika hizi mobile operators. Nafikiri kuna 10% pengine ndio maana hawa jamaa voda tigo airtel nk. hata hawaogopi TCRA, ni kama jibwa pole. Kiberiti ni sh 50 tu lakini kiwanda cha kiberiti pia ujue kina Mkurugenzi yaani Director General lakini huwapenda walaji na kuhakikisha kiberiti kinakuwa kile kile mpaka uzeeke. Na anaheshima zake katika jamii. Lakini kama utakuwa mkurugenzi TCRA sisi tutajivunia nini watanzania haswa katika swala zima la mobile phone operators;
  1. kutuma msg zisizo msingi kwa wateja na kwa idadi hadi kuwa usumbufu/kero kwa mtumiaji .....TCRA kimya
  2. Customer care zote --holding up to forever without assistance na TIGO naambiwa huchaji customer care sh 50 per connection ....TCRA kimya
  3. Kuchezesha kamari katika simu za mkononi wakati nchi maskini ...TCRA kimya
  4. Mawasiliano kuwa si mazuri hasa voda kwa sasa ...TCRA kimya


  TCRA igeni basi TBS wameridhia CoC au sijui PVoc ili kumlinda Mtanzania asipate bidhaa kama za mobile operators hapa nchini nyie je mtatulindaje. Nafikiri mobile operators nyie toeni licence na quality of their product ifannye na TBS. Sasa hivi naanza kupata imani nao sana.

  Naomba kuwakilisha kero zangu hapa hapa.
  Asanteni kwa kunisoma.
   
 7. killo

  killo JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 393
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  mijitu mingine bana.... Kama namuona huyo mhusika huko TCRA kehspewa vx tumbo limemsimama hata kazi hawezi kufanya tena anakula raha tuu tanzania yoote yake.... Fanyeni kazi yenu bwana muache ujinga si tunalipa kodi nyingi sana kwaajili yenu msituhanithi hapa mxiiiiiiii...!!!
   
 8. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #8
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Tunaimani na JF kuwa ni moja ya njia ya kufikisha malalamiko yetu kwa wahusika.
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Hilo kweli, mimi situmii TiGo kupiga simu zangu, natumia modem yao kwa internet tuu, lakini juzi ndio nimeamini kuwa 1) wizi na 2) waongo. Natumia kifushi cha max na bahati nzuri kimekwisha kabla ya mwezi, ingawa wao wanasisitiza kuwa hata 1.5gb wanazokupa zikiisha utaendelea kutumia modem. Cha kushngaza ni kuwa kweli, unaingia kwenye internet lakini site zote hupati, wantazama trend yako tu, na wanakuwachia sites kama za email na JF pekee. Hupati hata wikipedia, hupati chochote ukitafuta kutokea google.

  Huu ni wizi wa waziwazi. Si wangesema tu, zikiisha nunuwa kifurushi kingine, kuliko kuwacha tunahangaika kutafuta ushauri, labda PIPA, labda mtandao mbovu, labda websites zimefungwa, yaani wanachofanya ni kitu kibaya sana tena sana, Na nikijia mjini nanunua modem nyingine na kadi yao naivunjavunja na kuitupilia mbali, naomba na wengine wafanye hivyo. Dawa yao haya makampuni ni kuwasusia tu.
   
 10. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  Tigo ni kakampuni kadogo tu kilichojiingiza kwenye ushindani na makampuni makubwa tajiri. Sasa kamefulia na kuamua kuwaibia hadi mahousegirl wa watanzania. Toka tigo waanze wizi wao wa kutumia nguvu imepita kipindi cha karibia mwaka sasa sababu walibadilika ghafla baada tu ya kikao cha bajeti cha 2011/2012. Wateja wamelalamika na kwa sababu awamu hii ni kama hatuna serikali hapakupatikana wa kuwasaidia malalamiko yao. Line ya tigo mie niliitumbukiza ndani ya jiko la mkaa siku nyingi.
  .
   
 11. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,317
  Likes Received: 2,283
  Trophy Points: 280
  Umenena,asubuhi hii bundle yangu ilikwisha lakini hiyo nyongeza wanayosema waliondoa ikabidi ninunue nyingine...huduma zao mbovu sana,ukipiga customer care mpaka wapokee ipo kazi na wakipokea uelewa wao wengi ni mdogo.Najaribu kufikiria kama umekosea Tigo pesa ukatuma kwa mtu mwingine hali itakuwaje..mpaka wapokee umeshaibiwa....ongeza na makato ya huduma kwa mteja aaaaaaagh.
   
 12. Ungana

  Ungana JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 358
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Promosheni zao sasa,wizi mtupu!
   
 13. m

  magicboy New Member

  #13
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kuna hii sms "1 New Info Msg" ukifungua inasomeka " NYIMBO BURE PIGA 15050" inaingia kila dakika siku nzima yaani mpaka kero! Customer care hawapokei simu!
   
 14. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #14
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Modem zao zinachakachulika pia, unaweza kutumia line zote. We download program inaitwa joinair 3g ya ZTE. Wataalamu watakuelekeza hata hapa JF wapo.
   
 15. G

  Gonza Member

  #15
  Feb 6, 2012
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Dear Customer,

  Thank you for your candid feedback. It is difficult for us to assist you without further details such as your number and time of occurrence of problem. Please include such information whenever you convey your concerns.
  Please note that every operator charges for calls directed to customer care to avoid playful calls and ensure only customers who have issues are served.

  We do have channels which you can utilize to raise your concerns free of charge. We have call centers and various locations and also a Facebook page where we provide the best and timely customer care services.

  Whenever you have any concern, query or suggestion, please convey it to us through our Customer Care tab on our Facebook page on www.facebook.com/TigoTanzania.

  Tigo
   
 16. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
 17. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Binafsi nashawishija kufikiri TCRA wanahusika ktk wizi huu dhidi ya watanzania maskini. Jambo hili limelalamikiwa na kupigiwa kelele sana bila hatua za kueleweka kuchukuliwa
   
 18. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #18
  Feb 6, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ndo tatizo lenu la degree abroad sasa watu wanatumia lugha nyepesi ya kiswahili na wewe umesoma umeelewa kwanini usijibu kwa kiswahili? You are doing marketing in Tanzania why complicating yourself with language? Have you noticed what kind of people you are dealing with? Can we have your CV first that qualified your position? Or just Godfather position.
   
 19. c

  caca Member

  #19
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Unalalamika nini mkuu? tatizo wtz mmezoeshwa vya bure. Hiyo ndo inatakiwa. kwa kawaida ukiconnect network yao lazima ulipie service charge fulani hata kama no. haipatikani. Nchi zingine mbona gharama hizo za kawaida eg. SA.  U
   
 20. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #20
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Binafsi nashawishija kufikiri TCRA wanahusika ktk wizi huu dhidi ya watanzania maskini. Jambo hili limelalamikiwa na kupigiwa kelele sana bila hatua za kueleweka kuchukuliwa
   
Loading...