TCRA ifumuliwe wawekwe watu wenye uwezo

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,308
6,884
Wote tunajua tatizo la utapeli mitandaoni, kero za simu na sms za kutapeli, wengine wamekwepa mitego wengine wamepata hasara.
Wote tunakumbuka taabu ya kupanga foleni NIDA kutafuta namba ili line zisifungiwe.

Katika taabu zile zote tuliaminishwa kuwa ndio itakuwa suluhisho la utapeli mitandaoni. Je utapeli umeisha? Kwanini zoezi lililoigharimu serikali na wananchi wengi fedha nyingi na muda wao limekuja kuwa bure na wanaohusika wapo maofisini tunategemea watupe tena suluhisho.

Kuna maswali ya msingi inatakiwa tupatiwe majibu kwa kina:
1. Unakuwaje na mfumo ambao wanaosajili line za simu(wakala) hawafahamiki? Kwanini wanashindwa kujua nani hasa anasajili line za matapeli?

2. Ili usajili line unahitaji namba ya NIDA na utaconfirm kwa kuweka kidole. Je wanaotumia namba za NIDA za watu wengine wanaweka kidole kipi kuthibitisha usajili?

3. Simu zote zina IMEI kwanini simu zinazofanya utapeli zisifungiwe kabisa kuweza kupata mtandao zaidi ya kufunga tu line?

4. Ushauri mwingine wa kupata mapato.Kwanini pasiwepo na kitengo maalumu ambacho kitashirikiana na polisi. Mtu akiibiwa simu akienda na vielelezo pawe na charges zinazofahamika mtu analipia na simu yake inakuwa tracked. Hii itapunguza wizi wa simu mitaani.

Naona bado TCRA hawajafanya vizuri kazi yao kama inavyohitajika.
 
Kiukweli ktk mambo ambayo jamaa wamefeli ni hilo la kudhibiti wazee wa 'ile hela'
 
Suluhisho ni hili

Mtu aruhusiwe kumiliki SIM kadi 1 tu kwa kila mtandao. Na hiyo namba iwe kama TIN haiwezekani badilishwa, ukifa na yenyewe inakufa.

Namba itayobainika kufanya utapeli ifungiwe yenyewe na kitambulisho ili asiweze pata mtandao mwingine.

Kila mtu awe liable na matumizi ya SIM kadi na Simu
 
Back
Top Bottom