TBS yatoa tahadhari kuhusu maziwa ya watoto aina ya SMA

TBS yatoa tahadhari kuhusu maziwa ya watoto aina ya SMA

ChekoFagia

Senior Member
Joined
Sep 20, 2025
Posts
115
Reaction score
339
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kuutaarifu umma kuwa mnamo tarehe 06 Januari 2026, Kampuni ya Nestlé nchini Uholanzi (Netherlands) ilichapisha katika tovuti yake taarifa ya kusitisha na kuondoa sokoni matoleo (batches) kadhaa ya bidhaa ya maziwa mbadala ya watoto wachanga (baby formula) aina ya SMA katika soko la dunia (recall notice). Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na tahadhari ya uwezekano wa kuwepo kwa sumu aina ya Cereulide.

Sumu ya Cereulide huzalishwa na vimelea vya Bacillus cereus na inaweza kusababisha kichefuchefu, kutapika pamoja na maumivu ya tumbo.

Aina ya maziwa hayo ya SMA yanayohusishwa kuwa na kichafu hicho ni: SMA Advanced First Infant Milk, SMA Advanced Follow-On Milk, SMA Anti-Reflux, SMA Alfamino, SMA First Infant Milk, SMA Little Steps First Infant Milk, SMA Comfort na SMA Lactose Free.

TBS inapenda kujulisha umma kuwa matoleo (batches) yaliyoelezwa tahadhari hayajawahi kusajiliwa hapa nchini. Hata hivyo, kutokana na hatua iliyochukuliwa na Kampuni ya Nestlé, TBS imechukua hatua za tahadhari (precautionary measures) kwa kuendelea kufuatilia ukaguzi katika soko na kuimarisha uagizaji katika vituo vya mipakani ili kuhakikisha kuwa maziwa hayo hayajaingia nchini.

Aidha, TBS inatoa tahadhari kwa wananchi kuto nunua, kutumia au kumpatia mtoto bidhaa yoyote ya SMA ya aina zilizotajwa hadi hapo itakapotolewa taarifa rasmi nyingine. Vilevile, wananchi wanahimizwa kutoa taarifa mara moja kwa TBS endapo watakutana na bidhaa za SMA za aina zilizotajwa katika taarifa hii.

Kutokana na taarifa hiyo, TBS inawaonya waagizaji, wasambazaji na wauzaji wote wa bidhaa za maziwa mbadala ya watoto kuwa ni marufuku kuingiza, kuuza, kusambaza au kumiliki bidhaa zozote za formula za watoto ambazo hazijasajiliwa na Shirika la Viwango Tanzania. Viongozi wote watakaobainika kukiuka agizo hili watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Viwango, Sura ya 130.

TBS inapenda kuwahakikishia umma kuwa itaendelea kulinda afya, usalama na maslahi ya walaji kwa kuchukua hatua stahiki bila kusita dhidi ya mtu au taasisi yoyote itakayokiuka sheria na taratibu za viwango.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali piga namba ya bure: 0800 110 827.
1767963790065.png
 
Vipi haya maziwa yetu ya humu humu nchini yote yana viwango vya tbs au wananchi wanajinyea tu bila kujua kama yana sumu hiyo? Maana kuna maziwa ukinywa lazima ujisikie kichefuchefu na kutaka kutapika, isije ikawa yana bacteria hao wanaozalisha hiyo sumu!
 
TBS ni kama TMA tu, wanasubiri wakali wa standards wafanye uchunguzi wa kisayansi na kupata majibu halafu wao wanakopi na kutoa tamko kana kwamba wameingia maabara.

Kwa mtindo bidhaa feki haziwezi isha hapa Nyonyoland.
 
Back
Top Bottom