TBS na sukari kutoka nje, je mnalijua hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBS na sukari kutoka nje, je mnalijua hili?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiresua, Jan 19, 2012.

 1. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ni takribani miezi 6 tangu nilipomuuliza mwenye duka kwa nini hauzi sukari ya nje, 'Brazili' anauza ya Ilowo! Wakati sukari ya TZ ni ghali kuliko ya Nje. Alinijibu kitu ambacho sikukitilia maanani kwani sikukiamini. Aliniambia sukari ya nje huwa sio kamili ki-uzani! Ni mwezi uliopita kijana wangu alinunua sukari ya Brazili kwa bei ndogo kdg ya Tz, akapiga simu kwa duka analonunua bidhaa, kumuuliza mbona unauza sukari bei ghali? Alimjibu kwani ni ya wapi? Akamjib ni ya nje! Akamwambia ipime ndo utajua ni kwa nini. Oh! Ilikuwa pungufu kilo 10, yani badala ya kilo 50, ilikuwa ni kilo 40. Nikakumbuka maneno aliyowahi kuniambia. Sasa hi imekuwa ni kawaida kwa matani na matani ya bidhaa hi inayoingizwa hapa nchini kwa ujanja wa wafanyabiashara, na kutumia fursa kuwaumiza WaTZ. Wafanya biashara wengi wadogo hawajawahi kulijua hili ndio maana wanaenjoy punguzo la sh 2,000 wanaliwa sh 18,000. Swali langu ni kuwa hv hawa TBS na WMA wanalijua hili au na wao ni sehemu ya tatizo? Au mnahangaika na malumbesa tu? Wanapotuambia wanakagua bidhaa zinazoingia nchini wanakagua badhaa gani? Kumbukeni tunawalipa mishahara kupitia kodi zetu mtulinde halafu mnazurura tu mjini. Kama mnaingiaga humu mkamwambie bosi wenu muanze ukaguzi.
   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  TBS?
  Sijui wapo kwa ajili ya nani...
   
Loading...