TBL yaonyesha sononeko lake kuhusu kuongezewa kodi kinyemela

Serikali inayoongozwa na akili ndogo..

wanapandisha ushuru..garama za bia zinapanda..wanywaji wanapungua kampuni haigenerate pesa za kutosha..itashindwa kujiendesha..itashindwa kulipa kodi.. serikali itakosa mapato na ukizingatia Mapato makubwa ya serikali yanatokana bia.

Hapa wange hakikisha wanywaji wanakuwa wengi ili kampuni izalishe sana na makusanyo ya kodi yaongezeke...

"Kwanini Nchi yako ni Maskini? Sijui-JAKAYA M. KIKWETE(Rais wa Tz 2005-2015)
 
Kamwe tusitegemee deni LA taifa kupungua kwa mwwndo huh.serikal inaogopa kuongeza vyanzo vingine vya mapato hasa ktk makampuni ya madini na utalii maana sekta hizo zmegusa maslah yao.so wanaogopa kizidiscourage!!y kiwanda cha bia tu ndo kiwe kinanyanyaswa tu na wateja wake!?? Serikali yetu kifikra iko taabani.wizara ya fedha nayo imechoka IPO ICU.yaaan wakilala na kuamka wanawaza bia tu.
 
Mchawi wa matatizo ya Waafrika ni akili zao ndogo pamoja na elimu zao duni,Kwanini ninasema hivi?Kwasababu sisi Waafrika tunachagua viongozi wanaotupa ridhiki za leo tu mfano;nguo na chakula wakati wa kampeni.Hatuchagui viongozi kwa kuangalia historia ya utendaji wa,mafanikio yao na mitazamo pamoja na itikadi zao za kiuchumi.Next election tuwahamasishe Watanzania wenzetu kuwachagua Technocrats kuiongoza nchi,To hell with corrupt politicians! Tuwachague watu wenye background za kufanya biashara au kuwemo kwenye bodi za ukurugenzi/CEOs kwenye makampuni na mashirika ya ndani na ya kimataifa kwa mafanikio+uadilifu/uzalendo,Naamini hawa they have what it takes to manage the country's economy and steer it in the right direction.Hawa watu wakiwa viongozi wataona umuhimu wa kubana matumizi yasiyo ya lazima serikalini;watahimiza matumizi mazuri ya fedha za umma;ni results driven leaders;wataona umuhimu wa kuweka kodi nafuu kwa wafanyabiashara wadogo,wa kati na wakubwa;wataona umuhimu wa kuimarisha Huduma za maji,umeme na miundombinu ya usafirishaji kama vile barabara,Bandari,viwanja vya ndege na reli bila kusahau umuhimu wa kuiimarisha sarafu iwe na thamani.Wanasiasa hawajui umuhimu wa haya mambo katika kukuza uchumi wa taifa,wanachojali wao ni kutumbua pesa za walipa kodi tu basi.
 
ndo maan mtaani bia znapanda kila siku.yaaan hi serikari siku tbl na sbl vikiungua moto au kugoma kuzalisha kabisaaa hata week itakua hoi bin taaban. Siombei viungue maana tutakufa na kiu
kwa wanywa bia tu, natarajia kuamasisha mgomo endelevu wa kupunguza unywaji wa bia kwa kutokunywa bia kwa siku za ijumaa,j1 naj2 kwa muda wa mwezi 1 kwanza alafu tutafanya taathmini
 
Si tuna gesi na mbuga kaka?

Pamoja na yote hayo, vyanzo vikubwa vya mapato ya serikali hii legevu ni PAYE, pombe na sigara. Siku walevi na wavutaji wakiokoka basi serikali hii itaangukia pua. Niamini!
 
hao unaowaita walevi ndo wanakupa dawa hospital na pia ndio wanaochangia watoto wako wafundishwe shule, kwa ujumla ndo wanaifanya serikali yako ibaki hapo ilipo.
tena wanywaji inatakiwa waheshimiwe kwenye mabasi maofisini nk.tena mda wa kufungua baa na kufunga ufutwe wajiachiee ndo waendesha nchi hao ebo! Na wavutaji wasibughudhiwe popote pale
 
Bongo viongozi feki na wasomi wote feki. Bei ha crate la bia imepanda tena toka 35200 mpaka 36800 kinyemela. Hakuna mfumo wala utaratibu katika upangaji wa bajeti ya nchi hii. Poor bongoland.

Mkuu ni kwamba serikali imefulia hamna pesa hii leo tumekaa na katibu mkuu wa wizara yetu kujadili tunafanyaje kazi mishahara bado na sikuu ndio hiyo +wizara inamadeni mengi sana+OC kuchelewa yani ni kosa kubwa kurudia kuwapa kura watu wanaotuongoza!
 
Watengenezaji wa bia na vinywaji vikali, wametishia kufunga baadhi ya viwanda iwapo Serikali haitaipunguza ongezeko la kodi la asilimia 20 ... alisema uamuzi wa kupandisha kodi kinyemela umewaacha njiapanda wenye viwanda kwa kuwa ....

Wakati wa kuwasilisha Bajeti Waziri Mkuya alianisha kuwa Serikali ingepandisha bajeti ya Pombe kwa asilimia 10 % ...lakini kinyume chake Finance Bill ilivyotoka waziri alichapisha kuwa ongezeko kwa Pombe Kali ni asilimia 20. wenye viwanda wamelalamika Sana Juu ya uvunjaji Sheria huu ambao ni kinyume kabisa ......na hairuhusiwi kupindisha mambo ambayo yameshawasilishwa Bungeni ...

Upandishajii huu unahusishwa na ukosefu wa ubunifu wa Waziri na wasaidizi wake .....na kuwakomoa walevi .

___________________________________________________________
WAZIRI wa Fedha leo mjini Dodoma amesoma Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2014/15 ambapo bajeti hiyo ikiendelea kuwakamua watumiaji wa vileo (walevi), wapenda starehe pamoja na wavutaji wa sigara huku safari hii hauweni ikijitokeza kwa wafanyakazi baada ya kupunguza kodi za mishahara.

Akisoma bajeti hiyo, Bungeni mjini Dodoma Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (Mb) alisema ushuru wa bia inayotengenezwa kwa nafaka nchini na ambayo haijaoteshwa imepanda kutoka shs 341 kwa lita hadi shs 375, huku ushuru wa bia nyingine kutoka shs 578 kwa lita hadi shs 635.

_________________________________________

Alisema ushuru wa mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu ya nchini kiwango kinachozidi asilimia 75 imeongezeka kutoka shs 160 kwa lita hadi shs 176, ushuru wa mvinyo wa nje kiwango kinachozidi asilimia 25 umepanda kutoka shs 1,775 kwa lita hadi shs 1,953, huku ushuru wa vinywaji vikali ukipanda kutoka shs 2,631 kwa lita hadi shs 2,894.

-_____________________________________________________________

Ushuru Mpya

Excise Duty Rates For Soft Drinks, Beer And Wines



1.0

Soft drinks including mineral water

83 per litre



91 per litre

2.0

Locally produced fruit juices

8 per litre

9 per litre

3.0

Imported fruit juices

100 per litre

110 per litre

4.0

Beer made from local un-malted cereals



310 per litre

341 per litre

5.0

Other beers

525 per litre

578 per litre



6.0

Wine produced with domestic grapes contents exceeding 75%

145 per litre

160 per litre

7.0

Wine produced with more than 25% imported grapes

1,614 per litre

1,775 per litre

8.0

Spirits

2,392 per litre

2,631 per litre


Tanzania Revenue Authority - Summary of changes in tax laws administered by TRA as per budget 2013/2014
 
Makampuni yanafanya nayo siasa? Kodi si italipwa na mlaji? Malalamishi ya nini?
 
Na bado wapandishe hatutaki taifa la walevi.

Hutaki Taifa la Walevi Wakati mishahara wako ...au huduma unazopata ..Barabara..unayopita zote ni Kodi Za walevi.....

Hata Kama Hao mambulula wa Kikwete..WAMEAMUA Kupandisha kwa kukomoa walevi....,Hii Ina adhari kubwa kwenye Uchumi .....na pia kwa ustawi wa familia zetu

Kwanza viwanda vinalipa Kodi lakini havipewi huduma Za Msingi na Serikali Kama Maji na Umeme.....
 
Makampuni yanafanya nayo siasa? Kodi si italipwa na mlaji? Malalamishi ya nini?

Wewe Kasheshe hujui adhari ya ongezeko la bei kwa Mlaji...
1. Kuacha kutumia
2. Kutafuta substitute drink ...Matokeo ni kunywa Gongo wakaumia afya au kuchochea smuggling ambapo majirani wataingiza Pombe kwa Njia Za panya ....na kuuza vichochoroni .....

Mahitaji yakishuka ..uzalishaji tukashuka ..basi na Hiyo Kodi ya 20 % WATAKOSA

Lakini kikubwa ni kuwa katika Utawala Bora ...Kudanganya Bunge ni kosa kubwa na dharau ..ambapo Nchi nyingine Serikali hutakiwa kujiuzulu. ....
 
Lile bunge halina kazi yoyote, wanakula pesa zetu tu.Serikali inaongeza kodi kinyemela na inajua bunge limejaa wengi waganga njaa itawafumbia macho tu.
 
Bongo viongozi feki na wasomi wote feki. Bei ha crate la bia imepanda tena toka 35200 mpaka 36800 kinyemela. Hakuna mfumo wala utaratibu katika upangaji wa bajeti ya nchi hii. Poor bongoland.

Unategemea nini kama kiongozi wa nchi hana sense of economic direction bali kuongozwa na matukio?
 
Unategemea nini kama kiongozi wa nchi hana sense of economic direction bali kuongozwa na matukio?

Eti waziri anakomoa Walevi.....walevi wako dini zote ...na wala hawana nongwa na mtu ...wanalipa Kodi ....lakini Sasa watafute na mawazo mengine ..........na Hii yote inatokana na kamati ya Bunge kuwabana Sana kwa kuendelea Kuleta bajeti Za Pombe na Sigara ..hadi waziri akalia ..alivyotoka hapo kwa Kiburi akaamua kupandisha sio asilimia 10 % ambayo kamati ya bajeti waliona ni kubwa ...Bali kwa Asilimia 20 % kabisa ..kiburiiiii


Nchi zote ongezeko linalokubalika la Kodi ni kwa Kiasi kisichozidi Inflation rate ...au la Serikali kutafuta new source of revenue .......kwa mwendo huu wa kutokusheshimu bunge ..looo



https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-kujibu-hoja-za-kamati-alia-kama-mtoto-5.html

27 Jun 2014 - Waziri wa Fedha Amwaga Machozi Kweupe ... na Andrew Chenge, juzi kilimfanya Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya Salumu, Kumwaga chozi kikaoni. Waziri huyo alilazimika kumwaga chozi baada ya wajumbe wa ...
 
Back
Top Bottom