Tbccm?

jeviounipers

Member
Jan 5, 2011
68
26
Tokea bwana Tildo Mhando aondoke TBC1 imekuwa ya ajabu na ya hovyoo sana. Habari za muhimu za matukio muhimu hayaoneshwi tena na kituo chetu kipenzi cha TBC au ikitokea wameonesha basi ni kidogo sana as if it doesnt matter at all na utafikiri hazina kipaumbele chochote. Tena hususani zile habari za matukio yanayo elezea hisia kali za wananchi kwa serikali kutokana na ugumu wa maisha, manyanyaso ya serikali, maandamano ya amani, urudishaji wa kadi za chama tawala, makongamano ya CDM, maandamano ya wanafunzi, malalamiko ya bei za vitu kuwa juu n.k ndio hutakaa uyaone TBC . Kuna kipindi walikuwa wana session ya kusoma ujumbe mfupi wa maandishi unaotumwa na watazamaji katika taarifa zao za habari, lkn tokea Januari 5 (mauaji-arusha) ndio ilikua mwisho wa kusoma (sijui kama wameanza tena) maana siangalii tena TBC habari. Ule ujumbe mfupi ulikuwa unahaririwa kabla ya kusomwa, kama ni wa kuiponda serikali hawasomi, ukisifia utasomwa hata mara 3, sasa baada ya Mashujaa Day,January 5 wamepata kigugumizi, hakuna cha kuhariri tena kwa kuwa raia wana hasira na hakuna zuri linalosemwa na raia kipindi hiki cha udhalimu wa Siri-Kali ya Mkwere.
Pia kama kuna mtu anajua sababu ya Mhando kutoka TBC naomba aweke hadharani, maana nimesikia mengi sana ya utata kuhusu hili swala.
 
Wana JF Imefika mahali sasa TBC1 kukataliwa na kupewa fundisho kwa mambo yao ya kitoto kwani kama muhusika mkuu anakuchakachulia habari yako vp zile za mbali ambazo aujazishuhudia. mfano leo ktk maandamano ya Dodoma Chadema walikuwa wanapinga mauaji ya arusha, dowans na tume ya katiba ya Mkwere ila cha ajambu TBC1 wakasema ni maandamano ya kumuunga mkono Mkwere na tume yake ya katiba.
My take: TBC1 INAPOTOSHA JAMII NA DAWA SIO KUTOKUANGALIA ILA NI KUPAZA SAUTI ZETU NA KUWALAANI PINDI TUWAONAPO.
 
Chombo cha propaganda cha ccm,hakuna tofauti redio uhuru na magazeti yao, wamekwisha utaona muda si mrefu jamaa wanaangalia pa kwenda pamekwisha ingia ruba tbc 1,
 
haya mambo ya kilofa tuyakatae sasa tuwe tayari kufa tukitetea haki kuliko kuishi tukinyanyaswa
 
Back
Top Bottom