TBC2 mashindano ya Jumuiya ya Madola inawahusu

TBC2 mashindano ya Jumuiya ya Madola inawahusu

okaoni

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2011
Posts
1,471
Reaction score
1,308
Kwaza kabisa niwape pongezi nyingi kwa kutuletea michuano yoote ya kombe la dunia na marudio yaki ijapokuwa ilikuwa haituhusu. Hakuna timu hata moja ya ukanda wa Afrika mashariki na kati iliyokuwepi kwenye fainali hizo.

Ninajua TBC 2 iliundwa ili iwe ya burudani kuepuka kukatisha vipindi vingine vilinavyoendeshwa na TBC 1. (Tena hongereni kwa kupata gari la kisasa kabisa la pili Africa la matangazo)

Tuna vijana wetu wamekwenda Scotland kushiriki mashindano ya jumuia ya madola ijapokuwa walichaguliwa kabla ya mashindano ya riadha ya Taifa potelea pote ni watanzania wanatuwakilisha, tutawaonea wapi ili wasiambiwer tena walienda kutalii kama mashindano ya msimu uliopita yaliofanyikia India. Ni matumaini yangu kuwa kama mlivyochukua muda mrefu kuonyesha masindano yasiotuhusu ya kombe la dunia , mtakuwa wazalendo kabisa kutuonyesha vijana wetu wanafanya nini teeena mlete na wachambuzi wachambue kama mlivyofanya kwenye kombe la wazungu na wa amerika.

Nitashangaa sana kama hamtasikia kilio changu na kuendelea kupiga miziki ambayo tumeshaisikia na hata tunaweza kuisikiliza kupitia TBC Taifa au FM. Kama hii haitaonyeshwa nitaamini kuwa na ninyi mnashiriki kuiua michezo mingine na kukumbatia mpira wa miguu ambayo ilishatushinda. Ninatarajia mpatapo andiko hili basi mtaaza matangazo kwa fujo ya kuwaalika watazamaji wawashuhudie vijana wao wanavyo fukuz upepo na kushuhudia wimbo wa taifa letu penwa ukipigwa huku uskochi pale wanariadha wetu watakapo wazidi wanariadha wa Kenya na kujinyakulia medali. Wasalamu mimi mwenyewe
 
Back
Top Bottom