Tbc1 na uchakachuaji wa habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tbc1 na uchakachuaji wa habari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by babad, Jan 30, 2012.

 1. babad

  babad Member

  #1
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa TBC1 siwaamini kwani wamekuwa wanachakachua habari kwa kuondoa vipande wanavyoona vinaleta sura tofauti na matakwa ya serikali.Mfanno jana wameonyesha Dr.Mwakyembe na Sita wakitoa hotuba kanisani lakini wakakata sehemu ambazo wanaeleza juu ya yeye kunyweshwa sumu,leo wanasema madaktari wamerudi kazini na huduma zinaendelea vizuri kwa baadhi ya hospitali ila wanasema mikoani na Dsm hawaijumuishi kabisa.Kwa hali hii tuna haja ya kuiamini???
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,227
  Trophy Points: 280
  Babad, TBC ndio tv pekee yenye maripota maeneo mengi kuliko TV nyingine yoyote. Kwa vile hii ni TV ya taifa, lazima habari zake ziwe ni zile zenye maslahi ya kitaifa.

  Hivyo katika huu mgogoro unaoendelea TBC lazima iripoti kwa maslahi ya taifa .

  Kama hospitali ina madaktari 10 na wawili wamerudi kazini na 8 wamegoma, TBC itatangaza madakitari warejea kazini and they are right kwa sababu hayo ndio maslahi ya taifa kwao!.

  Hata hivyo vyombo vya habari vya kinataifa navyo vinaripoti kwa kutanguliza maslahi ya mataifa yao. Kwa wenye kumbukumbu mliona jinsi CNN walivyoonyesha miili ya watu waliokufa mauaji ya Rwanda, jinsi walivyomuua Saadam, Osoma na juzi juzi jinsi walivyouanika mwili wa Ghadafi.

  Lakini ni CNN hao hao hawakuthubutu kuonyesha miili ya hao wamarekani wanaokufa vitani wanakufaje!. Mwili wa mmarekani kwao ni maslahi ya taifa na kuonyesha dilapidated bodies za wengine kwao ndio habari.

  Hivyo TBC kwenye huu mgomo itatangaza mazuri na kuwajulisha madaktari na umma wa watanzania kuwa mgomo umeisha!. Hayo ndio maslahi ya taifa.

  Binafsi naungana na msimamo wa TBC na nimesikitishwa kwa jf to take sides kushabikia mgomo unaendelea!.
   
 3. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280

  pointless!!!!!!!

  Mizambwa
  inaniuma sana!!!
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,227
  Trophy Points: 280
  Ukishaweka pointless inasema na points zako ni zipi!.

  Pointsless ambazo nazo hazina points pia ni pointless, hivyo pointless ya pointless ni pointless!.
   
 5. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  tbc1 iko kwa maslahi ya serikali, sijaona tv ya kisenge km hii, full kurudia vipindi na hata wale jamaa zangu wa origin comedy nao wamegombana nao, mi sijui kwamba cku hz pale kunamkurugenzi au sharti maana nahisi waziri wa habari na utamaduni ndio editor wa vipindi vya tbc1, akisema hiki kisionyeshwa basi hamkioni.Pumbafuuuuuuuuuuuuu
   
 6. Achahasira

  Achahasira JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ningepuka like kama ningekuwepo kwenye pc,well said
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  pasco nilikuwa siamini kuwa umenunuliwa ila sasa kwa mbaaali naoana kama umenunuliwa tena kwaa bei ndogo kweli!
   
 8. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135

  Mkuu wewe ndo pasco mayala wa maonyesho ya mwalimu Nyerere?

  Ni bora ungekaa kimya kuliko kutokea kutetea TBC, kila mtu anajua udhaifu wa chombo cha habari. TBC ni media ya wananchi lakini haiwajulishi wananchi halihalisi ya madhara ya mgomo huu. Bila kuangalia upande ilibidi iwajulishe wantzania impact ya huu mgomo ili wajudge wenyewe. wangefanya hivyo wangeweza kuharakisha utatuzi wa huu mgomo kuliko kuficha hali halisi. Wakumbuke serikali inapashwa kufanya yaliyomatakwa ya wananchi na sivinginevyo. Kwa kuficha ukweli, mnawanyima wananchi kufanya maamuzi juu ya mgogoro huu. Serikali haina mamlaka ya kupandisha mshahara wa madaktari ispokuwa kwa ruhusa ya wananchi kupitia wawakilishi wao(wabunge). Kama serikali ilishapewa budget ya kufanya hivyo basi huu utakuwa ni msala wao lakini kama hawajapewa basi hawana haja ya kuzunguka ni kurudi bungeni kuomba fedha zaidi kwa ajili ya mgogoro huu kuliko kujifanya wao ndiyo wenyemaamuzi na kodi ya watanzania.

  Sijapenda unavyolinganisha CCN kwa maswala ya vita kati ya nchi na nchi, hilolikowazi kuwa media inapotoa habari dhidi ya nchi na nchi yake lazima haiwezi kureport kushindwa. Mgogoro huu ni kati ya watanzania na serikali yao hivyo TBC wanatakiwa kukaa katikati kama mpatanishi kwa kutoa habari zitakazo wafanya wananchi watoe maamuzi sahihi na kujua nani ni mwenye makosa kati ya pande mbili.
  Ukweli utabaki kuwa TBC ya leo siyo ile TBC ya TIDO !
   
 9. Hulbjd

  Hulbjd Member

  #9
  Jan 30, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  Jaman Itv ndo mpango mzima
   
 10. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Unadhani ni nani anataka yamtokee kama yalivyomtokea mkurugenzi wake Tido Mhando?Ni lazima wachakachue ili vitumbua vyao visiingie mchanga hata kamaukweli unajulikana wazi.
   
 11. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #11
  Jan 30, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Who defines the national interests? Why can they let us know everything and leave the judgement and analysis to viewers? Maslahi ya taifa kwao nini nini wakati wanatulisha matunda mwitu?
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,227
  Trophy Points: 280
  Ngonini, nakubaliana na wewe kuwa TBC ya sasa sio TBC ya Tido na labda ndio maana sasa Tido hayupo pale!.

  Tido alifuata misingi ya uandishi wa habari kwa kuigeuza TBC kutoka TV ya serikali (goverment media) na kugeuka TV ya umma. (Public TV).
   
 13. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #13
  Jan 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mara nyingi mimi huwa sipendi ligi, lakini unasemeaje hili:
  Kwa namna moja au nyingine ninalipa kodi ambayo, pamoja na mambo mengine, kodi yangu inatumika ktk kuiendesha TBC, kwa lugha nyepesi, mimi ni miongoni wa wamiliki wake. Sasa ukafika wakati, nahitaji kupata habari (ambayo kwanza ni haki yangu kikatiba), kwa nini hiki chombo changu kisinipe habari sahihi?

  Lakini pia, nini maana ya habari sahihi, kwa kufunika funika mambo, ndio kunafanya habari iwe sahihi? Lakini pia, unadhani kuna mwananchi ambaye hana haja na kujua mgomo huu unaoendelea? Unaonaje ndugu yangu kama unefafanua madhara yatakayotokana na wananchi kujua ukweli kuhusu mgomo huu?
   
 14. afrolife

  afrolife Senior Member

  #14
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 45
  ... uko uchi mkuu, jisitiri japo kidogo!!
   
 15. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #15
  Jan 30, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,689
  Trophy Points: 280
  Pasco heshima kwako. Nimeyapenda na kuyakubali maelezo yako yaliyojaa rundo la facts na hikma.
   
 16. M

  MWENDAKULIMA JF-Expert Member

  #16
  Jan 30, 2012
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 961
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Sijaona "hikma" yeyote hapo.Kulinganisha CNN inavyoreport kwenye vita na TBC1 inavyoreport mgomo wa madaktari watanzania dhidi ya serikali ya Tanzania!
   
Loading...