Babad, TBC ndio tv pekee yenye maripota maeneo mengi kuliko TV nyingine yoyote. Kwa vile hii ni TV ya taifa, lazima habari zake ziwe ni zile zenye maslahi ya kitaifa.
Hivyo katika huu mgogoro unaoendelea TBC lazima iripoti kwa maslahi ya taifa .
Kama hospitali ina madaktari 10 na wawili wamerudi kazini na 8 wamegoma, TBC itatangaza madakitari warejea kazini and they are right kwa sababu hayo ndio maslahi ya taifa kwao!.
Hata hivyo vyombo vya habari vya kinataifa navyo vinaripoti kwa kutanguliza maslahi ya mataifa yao. Kwa wenye kumbukumbu mliona jinsi CNN walivyoonyesha miili ya watu waliokufa mauaji ya Rwanda, jinsi walivyomuua Saadam, Osoma na juzi juzi jinsi walivyouanika mwili wa Ghadafi.
Lakini ni CNN hao hao hawakuthubutu kuonyesha miili ya hao wamarekani wanaokufa vitani wanakufaje!. Mwili wa mmarekani kwao ni maslahi ya taifa na kuonyesha dilapidated bodies za wengine kwao ndio habari.
Hivyo TBC kwenye huu mgomo itatangaza mazuri na kuwajulisha madaktari na umma wa watanzania kuwa mgomo umeisha!. Hayo ndio maslahi ya taifa.
Binafsi naungana na msimamo wa TBC na nimesikitishwa kwa jf to take sides kushabikia mgomo unaendelea!.