Ukweli ni kwamba TCB One, TBC Taifa na Matibii yote yanakera! Mi nadhani CHADEMA wangewaandikia barua kuwaambia waache kutangaza habari zao kwa sababu wanayoyafanya ni mambo ya kipuuzi sana. Kwenye Radio yao asubuhi wana kipindi kinaitwa Asubuhi Hii. Hiki kipindi kinaanza na taarifa ya habari. Robo ya muda wa taarifa ya habari wanaongelea Kampeni za JK, halafu wanafuatia habari za CUF kama dakika mbili na nusu. Habari za Kampeni za CHADEMA hazizidi nusu dakika. Baada ya Taarifa ya Habari wanaanza kutangaza Habari mbali mbali, kimsingi hapa wanarudia zile habari walizozitangaza kwenye Taarifa yao ya habari lakini hapa wanaongea kirefu wakirudia 'madudu' ya JK. Kwa mfano wiki hii Topiki kubwa za JK ni Umwagaji Damu, Udini na Elimu ya bure. JK anazunguka na mtangazaji mmoja anayefanya kazi TBC kituo cha Songea anaitwa Gershon Msigwa. Huyu jamaa anatangaza kwa mbwewe hivyo kapewa tenda ya kuzunguka na JK ili mbwewe zake ziweze kuwateka wapuuzi wenzie. Naona Marin Hassan kapigwa chini! Mimi siungi mkono wale wanaosema CUF ni CCM B lakini ukweli TBC wamakuwa wakiipa CUF muda mwingi baada ya ule wa CCM. Yawezekana kwa sasa CUF si tishio tena kwa CCM au yawezekana wale wapuuzi wanatangaza habari za CUF wakidhani CUF watagawana na CHADEMA kura za kutoka upinzani au wanaidanganya jumuiya ya kimataifa kuwa wako 'fare' Juzi mtangazaji wa TBC One alisema, "Mgombea huyo wa CHADEMA alitumia muda mwingi kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe"!
Kichekesho kinakuja wakati wa kusoma vichwa va habari magazetini. Kama kuna habari habari zinazoelezea Kampeni za Chadema zilizoandikwa na magazeti basi utasikia mtangazaji akisme, "Nikilichukua gazeti la Tanzania Daima ukurasa wake wa tatu linasema ....." Yaani anaanza kusoma ukurasa wa tatu. Sasa akamate gazeti kama Uhuru, au Habari Leo au Jambo Leo (Hivi ni la nani hili?) utasikia, "Ukurasa wa kwanza wa gazeti hili JK afunika Songea, asema atanunua Meli inayotembea Nchi Kavu, Atajenga Hospitali yenye ghorofa 400 pale Mpitimbi, Ukurasa wa pili kuna picha inamuonyesha mgombea wa CCM Jakaya Kikwete akimbusu mama mmoja ambaye ni Mlemavu wa miguu (mtangazaji anachombeza kwa kusema 'ama kweli huyu ni kiongozi wa watu') nikiangalia ukurasa wa nne wa gazeti hili, kesi ya ugoni wa Slaa mambo hadharani kesho, ukurasa wa nane, mgombea mwingine wa Chadema azomewa mbele ya Slaa" Itaendelea hivyo hivyo hadi mwisho.
Sasa baadaye kuna SMS kutoka kwa wasomaji! Unaweza KUTAPIKA kama una roho nyepesi. "JK songa mbele baba ushindi tayari" na "Hao wanaotangaza kumwaga damu wanajisumbua" na "Waache watumie udini lakini mwisho wa siku hatuwapi nchi watake wasitake" na "Shimbo wewe ni mwanaume wa shoka kama hawakukuelewa waambie wasubiri" na "Hata mfanye nini ushindi ni kwa dk S..." Mtangazaji atakatisha hapa na kusema "Samahani msikilizaji ujumbe huu naona umefutika maana hausomeki vizuri"
Jamani viongozi wa CHADEMA kama mnanisikia mwambieni Tido aaachane na CHADEMA!