Mwanamageuko
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 8,604
- 5,581
Televisheni ya TAIFA TBC inapokuwa ikirusha wimbo wa hayati Remmy Ongala unaofahamika kwa kama "DODOMA" kuna maneno kama vile "ni yetu wenyewe.... WANACCM" hapo najiuliza hivi ndugu yangu Ayub Ryoba na wasaidizi wake bado wanadhani karne hii nchi hii ni ya CCM au inajengwa na wanaCCM pekee?
Bado katika mazingira kama hayo kuna jambo limekuwa likisemwa sana humu kwenye mabandiko kadhaa, tumeandika mara kadhaa lakini inaonekana ni kama tunajaribu kumuamsha mfu. TBC ni chombo cha Watanzania wote lakini kimekuwa kikitumika kisiasa zaidi na kama sehemu za kufanyia kampeni kwa chama tawala. Hapa itambulike haitutendei haki Watanzania kwani asilimia kubwa si wanachama wa vyama vya siasa na kama ilivyo asilimia kubwa pia si wafuasi ama wapenzi wa hicho chama chao.
TBC inapotumika kuhoji wakimbizi, viongozi wa dini wanaowataka wao pia kuonesha picha za wakimbizi inamaanisha nini? kwa wenye akili lile ni tishio la amani ina maana kuna mipango inafanyika ya kuvuruga amani ambayo wao TBC wanaijua. La si hivyo waseme wamekosa ubunifu ndio maana wanatisha watu badala ya kuonesha matatizo, changamoto na zinatatuliwa vipi ili amani iendelee kuwepo.
Kimsingi TBC wanasahau kuwa kote kusiko na amani chanzo chake ni tawala kushindwa kutatua matatizo ya wananchi wake, ama watawala kushirikiana na wageni kuwakandamiza raia wao na pia serikali nyingine kuchochea zenyewe chuki toka kwa watu wake kwa namna mbalimbali ikiwamo kutotaka kusikiliza kilio, changamoto na matakwa ya raia wao, huku viongozi na watawala wakitaka kulazimisha mambo yaende watakavyo wao bila uwezeshi ama ujenzi mazingira husika na rafiki katika kutimiza malengo. Katika hili wanapaswa kujirekebisha la si hivyo wataendelea kupoteza watazamaji ilhali wana vifaa kuliko vyombo vingine na huku wakila kodi za wananchi bila manufaa.
Tusipoangalia
"TUTAKUWA SAWA NA KASUKU ALIYE KATIKA TUNDU KILA APIGAE HODI HUITIKA KARIBU BILA KUWA NA UWEZO WA KUFUNGUA MLANGO!!"
Muwe na Jumatatu njema.