leonaldo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 2,584
- 3,185
Nianze kwa kuenda moja kwa moja kwenye hoja ya msingi.
Nichukue fursa hii kuvipongeza vituo binafsi vya television kuona umuhimu wa kuanzisha vipindi vya masomo ya shule kwa ajili ya watoto wetu walioko majumbani kwa sasa, ingawa jukumu hili kimsingi ni la television ya taifa.
TBC ni taasisi ya habari inayomilikiwa na umma, kwa maana ya kuendeshwa kutumia kodi za Watanzania, lakini kwa bahati mbaya TBC inaendeshwa kama chombo cha propaganda za kisiasa. Nasema hivi: Iko wazi kuwa haitoi haki sawa kwa wadau wa siasa hapa nchini na iko tofauti kubwa ukiilinganisha na mashirika mengine yanayofanana nayo kama BBC, VOA, DW na mengineyo yanayoendeshwa kwa kodi za wananchi.
Kwa sasa tunawaomba mpumuzike kwanza na kazi ya propaganda za kisiasa fanyeni kazi ya kusomesha watoto wetu na sababu zipo.
Kutokana na janga la ugonjwa wa corona shule zote zimefungwa na watoto wako nyumbani wanahitaji kuendelea na masomo.
Kama zinavyo Fanya nchi zingine duniani kusomesha watoto kwa njia ya mtandao watanzania hatuna uwezo huo.
Njia rahisi na inayowezekana ni kusomesha kwa njia ya TV live class program
Kwanini TBC au Safari channel
Ndiyo channel Pekee hapa nchini zinazo patikana nchi nzima kwenye ving'amuzi vyote na hata kwenye dish kubwa za kizamani bila malipo.
Radio ya taifa pia itumike sambamba na TV kufanya kazi hii isiyoepukika kwani hapo miaka ya zamani kazi hii ilikuwa inafanyika, nadhani hata vipindi bado mnavyo Kama hamjavitupa. Kwa hali hiyo uzoefu mnao na hata mahali pa kuanzia papo. Napendekeza iwe kama ifuatavyo:
TBC 1 na Radio masomo ya shule za msingi
TBC 2 masomo ya sekondari pia ifanyeni kuwa free na iruhusiwe kwenye ving'amuzi vyote
Safari channel, masomo ya high school.
NB: Masomo yaanze asubuhi hadi saa kumi, wizara ya elimu itoe waalimu. Naamini kama hamtanipuuza mtalisaidia taifa kuliko mnavyofanya sasa.
Povu ruksa