Tbc ni janga la kitaifa - boring

Tbc ni janga la kitaifa - boring

kisinja

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2013
Posts
243
Reaction score
297
Kwa kwel tbc imepoteza hadhi yake. Nimesikitika sana kuona mjadala wa sheria ya kura ya maoni unapamba moto kwa wabunge mahiri kutoa hoja za msingi kabisa lakini wakasema sauti ktk ukumbi wa bunge imekata na mafundi wanaifanyia kazi
wakati makinda anasimama kuahirisha bunge eti wanasema bila aibu kuwa sauti imerejea na spika akasema naahirisha bunge hadi kesho asubuhi. Dah watanzania sijui lini tutathaminiwa na serikali yetu kwa kodi tunayotoa kuendeshwa tbc lakini wakifanya mambo ili kukidhi matakwa ya watu fulani fulani.
Hofu yangu tumeingia ktk mfumo wa demokrasia ikiwa bado serikali yetu haiko tayari kwa baadhi ya mambo kama yaliyotokea tbc wakati wa mjadala wa jioni ya leo.
 
tatizo sio TBC.ni bungeni kwenyewe ndo wamecheza sarakasi

Leo mchana baada ya kuahirisha bunge wakaweka wimbo wa CCM. Nimewadharau sana, hata kama ni kujikomba kwa bosi, hii sasa ni too much.
 
tatizo sio TBC.ni bungeni kwenyewe ndo wamecheza sarakasi

Hizo sarakasi zinaanza tu mara baada ya hoja
za msingi kuanza???Haya yote yanamwisho wake. Huu ni ukiritimba kwa masuala muhim ya taifa kurushwa na moja tu. sasa bunge la katiba nadhani hata magazet yanaeza zuiliwa kuandika
 
wakuu, zile nondo zilizokuwa zikishushwa na mnyika na wenje,kafulila ziliwachanganya hadi wakaamua kuzima mitambo. shame on magambatv.
 
Tbc hawakuzima sauti mkuu,shughuli ilisimama baada ya mic za bunge zote kuzima,,bora ungesema mic za bunge ni janga la kitaifa tungekuelewa!
 
Hahhahaaa mic hizo hizo zilivyo smart zikarejea mara tu spika anapotangaza kuahirisha bunge!!!Duh bado tunasafari ndefu ya kufikiri
 
Siwatetei TBC lakini wao wangerusha nini kama spika anasitisha kazi mkuu?Na kama ni hujuma wao hawahusiki maana hawa control mfumo wa sauti bungeni
 
Poleni sana.tbc mwisho wao 2015 cdm ikiingia ikulu.tido atarudi
 
Nani kakulazimisha kuangalia??? Mbona kuna channel nyingi sana! Usiilaumu TBC jilaumu wewe na umaskini wako wa kingamuzi. Hamia DSTV!
 
mie namshukuru sana Mungu TBCCM haishiki kwangu, so sina presha
 
ukitaka kupunguza maumivu geuza antena yako
 
Kwani hamfahamu tunaendeshwa siri-kali iliyokubuu kwa kutaka kuutokomeza upinzani? Ndio maana mfumo wake mzima pamoja taasisi zake zimewehuka!
 
Mkuu TBC Ipo DSTV ktambo sana tatizo siyo kuhama bali kuacha kabisa kuangalia TBC.

Nani kakulazimisha kuangalia??? Mbona kuna channel nyingi sana! Usiilaumu TBC jilaumu wewe na umaskini wako wa kingamuzi. Hamia DSTV!
 
Kwa kwel tbc imepoteza hadhi yake. Nimesikitika sana kuona mjadala wa sheria ya kura ya maoni unapamba moto kwa wabunge mahiri kutoa hoja za msingi kabisa lakini wakasema sauti ktk ukumbi wa bunge imekata na mafundi wanaifanyia kazi
wakati makinda anasimama kuahirisha bunge eti wanasema bila aibu kuwa sauti imerejea na spika akasema naahirisha bunge hadi kesho asubuhi. Dah watanzania sijui lini tutathaminiwa na serikali yetu kwa kodi tunayotoa kuendeshwa tbc lakini wakifanya mambo ili kukidhi matakwa ya watu fulani fulani.
Hofu yangu tumeingia ktk mfumo wa demokrasia ikiwa bado serikali yetu haiko tayari kwa baadhi ya mambo kama yaliyotokea tbc wakati wa mjadala wa jioni ya leo.

Ukitaka kujuwa ubora wa TBC fananisha na chama tawala (CCM) ndipo utapata jibu sahihi. Sina la zaidi ya hilo!
 
Nani kakulazimisha kuangalia??? Mbona kuna channel nyingi sana! Usiilaumu TBC jilaumu wewe na umaskini wako wa kingamuzi. Hamia DSTV!

hiyo Dstv wanaonyesha bunge,? jaribu kutumia ubongo wako kidogo tu.!
 
TBC kama chombo cha ccm hawaruhusiwi kukava mikutatano ya vyama vingine. Bora wangemuacha tido zaidi kidogo.
 
Back
Top Bottom