TBC na Azam mnakera sana

mikedean

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
3,255
4,599
Yaani nao wanatumia video za youtube tulizostream jana na wao wanaoonesha kwenye habari hivyo hivyo halafu zinascrach. Hovyo sana na aibu kwa taifa hili la Tanzania. Yaani nao wanamtumia Dr Egy.net wanastream kwa very low quality wanatuletea na sisi hii ni aibu.

Kipindi cha 2015 kurudi nyuma TBC ilikuwa kipaumbele kwenye michezo saa hizi ni takataka. Hata utangazaji wao ni hovyo wa mechi za live. Ukiwa huku Mbeya haisikiki. Yaani mimi nikitaka michezo basi Abood FM ndio kiboko yao katika kutangaza.

Azam wananikera kwa sababu wanakaa Kwenye basi lao Dar wanafunga madishi yao halafu wanasema tupo Cairo stadium tunakuletea live. Bora nao wapewe changamoto ili wasitudanganye kama jana. Kama supersport wanarusha ligi ya zambia basi hata sisi tuwape na wao ili tuwachangamshe azam.

Kibongobongo pamoja na mazuri ya azam ila bado sanasana hasa kiutendaji kuna kitu hawako sawa.
TBC Waombe kibaki wauziwe mechi na azam hasa za timu ya taifa.
Ni hayo tu nimechoka hata sielewi.
 
Pamoja na mapungufu ya Azam hivi unaamini TBC wanaweza kuonesha mechi vizuri kuliko Azam? TBC wako vizuri kiutendaji kuliko Azam? Kutooneshwa mechi ya jana kosa la Azam ni kutangaza kuwa wataonesha halafu hawajaonesha, Wangesema tangu mwanzo kuwa hawataonesha sidhani kama ungewaanzishia mada.
 
TBC wanashindwa hata kuonyesha mechi za timu ya taifa,,
Yani timu ya taifa inacheza mashindano ya kimataifa wao hawana mpango kabisaa
Azam nafuu sana,tena sana tu
 
Pamoja na mapungufu ya Azam hivi unaamini TBC wanaweza kuonesha mechi vizuri kuliko Azam? TBC wako vizuri kiutendaji kuliko Azam? Kutooneshwa mechi ya jana kosa la Azam ni kutangaza kuwa wataonesha halafu hawajaonesha, Wangesema tangu mwanzo kuwa hawataonesha sidhani kama ungewaanzishia mada.
Wacha kiwatetea azam,hii sio mara ya kwanza kuwadanganya wateja wake utakumbuka yale mashindano ya Africa yaliyofanyika Misri baada ya Tz kutolewa na wao wakakata kuonyesha mpira, sisi tunaofatilia soka tunaboreka sana na azam wanapotudanganya tulipie king'amuzi chao alafu mpira hawaonyeshi na hii ni kwa sababu ya kudandiadandia vya rahisi na bure matokeo yake wanachinjiwa baharini dk za mwisho
 
Kweli Azam tv anahitaji mpinzani ili aongeze ubora

ukiwa unaangalia mpira kwenye Tv unaona kama wanatumia kamera moja..
 
Natumia dish la azam,kinachonikera ni kuweka sauti watangazaji wa bongo wakati nawao wanaangalia kwenye TV, jambo asipoliona vizuri anasubilia marudio,game inakuwa inakosa mvuto kabisa.......game za La liga hasa zinazohusu Real Madrid na Barcelona...... Wanatia kinyaa kabisa,acheni watangaze wenyewe
 
Kuna option ya kubadili lugha kwenye remote yako
 
TBC kuna kipindi kimoja tu, AKILI!

Back
Top Bottom