Jamani TBC duh yani kweli mnachakachua habari za Za wapinzani makusudi!Jana niliona Wametoa habari za slaa lakini wameichakachua kwakukwamisha CD makusudi kwakisingizio mitambo!!kwa maana hiyo kilichokuwa kikisemwa hakikusikika kabisa lakini TBC wajue ile ni pesa ya walipa kodi hata Slaa inamhusu mojakwamoja!!Badlikeni!
Nikweli hata mimi niliona pia za kikwete zilisumbua, Nadhani ni kweli wanamitambo mibovu!Mhh hapana sidhani kama ilikuwa ni lengo la kumhujumu Dr Slaa, kwani baada ya habari za Dr Slaa kukwama, zilifuatia za JK, ambazo nazo zilikwama, hadi ikabidi kwanza warekebishe na wakazirudia habari zote ya Dr Slaa , JK na Prof Lipumba na zote zikatoka bila tatizo. Jamani tuwe wakweli kiasi fulani.
Kwa jana, kama kuna mgombea atalalamika kuhujumiwa basi ni prof . Lipumba kwani walionyesha msafara wake tu mpaka hospitalini na malalamiko ya mpiganaji wa vita vya dunia. Lkn alipo anza kunadi sera zake tu mitambo ilianza nongwa.
Kwa jk sikuona tatitizo lolote, aliselebuka, akahutubia na alisikika bila shida. Na hata dr slaa pia alisikika.