Duh kumbe hili linagusa wengi, kwakweli TBC wanatuma kufanya kampeni za CCM kwenye mchakato wameenda mbali zaidi hata watu wanaojidai kuwahoji mitaani nao ni CCM. Kiukweli wanashindwa/kwa makusudi hawataki ku balance story. Hovyooo, tena bora yule cjui nani aliekuwepo mwanzoni kwenye kipindi cha jambo Dodoma alikuwa anahoji maswali ambayo CCM wanatakiwa kujibu.
Lakini huyu Mama ni kama sanamu kaletwa pale hana mbele wala nyuma, huu wizi wa kodi zetu kuna siku mtazilipa bila kupenda.
Jamani hiki Chombo cha utangazaji kinachojiita Cha Umma kimepoteza sifa ni bora kiitwe chombo cha CCM.Nasema hivyo kwa sababu hakitendi haki kwa watanzania kwa mfano vipindi vingi vya mahojiano kama Jambo asubuhi wanaohojiwa ni makada wa CCM hasa ktk Mchakato wa katiba mpya.Wanachokifanya wanachukua kada wa CCM na wajumbe wale 201 ambao ni makada wa CCM mfano Kingunge na kuanza kuendesha mdahalo juu ya katiba mpya.Jambo ambalo linakuwa limeegemea upande mmoja.
Mie Sina chama lkn kitendo hiki kinachofanywa na TBC hakikubaliki kwani hili shirika linaendeshwa kwa kodi zetu ikiwamo kodi yangu.Mfano mzuri ni hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa kufungua bunge imerudiwa zaidi ya mara kumi,cha kushangaza hotuba ya jaji warioba haikurudiwa kama ya rais,wakati ya warioba ndiyo ilibeba sauti kuu ya watanzania. Hata taarifa za habari ziko katika mlengo wa CCM.Sikatai kuwa hotuba ya rais isirushwe bali ninachokisema ni kuwa kuwe na msawazo ktk kurusha habari.Igeni mfano wa STAR TV na ITV wanajitahidi kuweka check and balance ktk midahalo yao.
Napendekeza hiki chombo kibadilishwe jina na kisiwe Shirika la Utangazaji la Taifa maana hakibebi maudhui ya watanzania bali kinabeba maudhui ya kisiasa zaidi.
You are very right.....Waache kwanza kutukata kodi...
ccm ni chama dola, chama pendwa, chama cha watu, hutaki unaacha
Leo tena TBC walikuwa na Mh
Nahodha na Bi Anna Tibaijuka. Hawasikii na wala hawakomi