TBC mko juu!

TBC mko juu!

mwita ke mwita

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2010
Posts
8,058
Reaction score
3,755
Nilianza kujua uwepo wenu kipindi mnaitwa TVT & RTD na PRT, kwa Kuiga nchi za wenzetu wenye SABC, UBC,KBC nanyi mkawa TBC, japo mnapokea ruzuku ya serikali ila mnafanya mambo si kwa faida ya watanzania mkiona TV nyingine zina program nzuri nyie badala ya kutafuta program nzuri nyie huamua kufanya kitu kiitwacho tukose wote, huwa mna wachukua waendeshaji au wahusika wakipindi hicho baadae wakija hapo kipindi kina kufa au kinapoteza mvuto

MAIGIZO YA KAOLE,kipindi hiki kilikuwa kinaonyeshwa na ITV siku za jumamosi na watu tulikuwa tunafurahi kuwaona waigizaji wetu wa kitanzania ambao walikuwa wanafanya vizuri kwenye Tasnia ya uigizaji maigizo maigizo kama TASWIRA, KIMBUNGA namengine matamu mkafanya hila mkawwaondoa Kaole Wakaja TBC baadae kipindi kikapoteza Mvuto watu wa maana kaole wakajitoe hadi leo hii watazamaji wamepungua kufuatilia maigizo yale.

ZE COMEDY, kipindi hiki kilianza na kilikuwa kinafanya kazi za ki fasihi, kuelimisha, kuburudisha na kuonya na watutulipenda hadi tukawa tunalipia soda baani ili tuangalie kipindi hiki, ikaonekana ITV wanafaidi mkawaleta hapo kwenu zaidi kinachoendelea na Komedi kinajulikana kwani hata mahausigeli siku hizi hawaangalii tena.

LIGI YA UEFA, nakaumbuka kipindi hicho nipo shule ITV na channel ten walikuwa wakionyesha mechi za UEFA kila jummanne na jumatano na tulikuwa tunafurahi baadae mkaingia kuonyesha UEFA, sijui kama bado mnaendelea kuonyesha kwani imebidi watu tutafute njia mbadala ya kuona UEFA baada ya mizinguo yenu.

LIGI YA UINGEREZA.

STAR TV walianza kuonyesha ligi ya Uingereza japo hawana ruzuku ila walikuwa wanajitahidi, baada ya ujio wa TIDO hapo TBC mkatutangazia kuwa Ligi itakuwa inaoneshwa, mlichofanya mkawa mnaonesha vitimu vidogo vidogo mechi kubwa hakuna, sijui kama bado mnaendelea kuonesha kama bado mnaendela hongereni

MANENO HAYO, kipindi hiki kilikuwa kizuri sana kilikuwa kinamuandaa msikilizaji wa Radio Tanzania asikilize taarifa ya habari mpaka sasa hatujui sababu za msingi za kuondoa kipindi kile kizuri.

MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI, kilikuwa kipindi kizuri sijui kama bado kipo.

Ninachokiona mbele kipindi cha wosia wa baba nacho mtakiondoa Kwa kweli mpo juu kwa kuua program nzuri na kutuachia ambazo mnafikiri zinawafaa kwa maslahi yenu
 
Ki ukweli TBCCM wako chini kabisa yaani wanashindwa hata na Sibuka TV!!
 
Hivi kile kipindi cha Jerry Muro kilipotea na Muro wake?
 
Mkuu umesahau kingine kikiitwa "SIPENDI" tbc fm
 
Tatizo la Tbc naona haina ubunifu hata mpira National Stadium Ligi Kuu inashindwa? Uncle Mnyika nako fuatilia 25 March 2013 utakapo kuwa Ikulu mnongoneze Mr President.
 
Jery Muro naye mapepe alichafua watu naye kachafuliwa.Kimbelembele kama Magufuri/Mwakyembe kutaka utukufu duniani kwa kuwaaribia watu wengine.Unafiki anakura jeuri yake.Acha bongo bwana.ukiwashindwa kula nao.Anayo bahati wangemnyofoa kucha na meno
 
jery muro naye mapepe alichafua watu naye kachafuliwa.kimbelembele kama magufuri/mwakyembe kutaka utukufu duniani kwa kuwaaribia watu wengine.unafiki anakura jeuri yake.acha bongo bwana.ukiwashindwa kula nao.anayo bahati wangemnyofoa kucha na meno
mtu akifanya vizuri anaitwa kimberembere,akibolonga fisadi,nchi imeoza.mafisadi wanasifiwa!
 
Hivi bado kuna watu wanaangali TBC?mi nilishaacha muda mrefu pamoja na kwamba inanasa kwenye king'amuzi changu,siangalii hata taarifa yao ya habari,hata iweje sitaki..
 
Jery Muro naye mapepe alichafua watu naye kachafuliwa.Kimbelembele kama Magufuri/Mwakyembe kutaka utukufu duniani kwa kuwaaribia watu wengine.Unafiki anakura jeuri yake.Acha bongo bwana.ukiwashindwa kula nao.Anayo bahati wangemnyofoa kucha na meno
Nimenusa harufu ya RUSHWA!, sijui kuna mla/mtoa hiyo kitu?. SIjui Sijui.................!.
 
Back
Top Bottom