Tbc kuwatumia kina masanja kuhujumu demokrasia.

Iga

Senior Member
Dec 17, 2007
112
6
HIVI leo kina Masanja, Joti, Mpoki na wenzao wanaanza KUTUMIWA na Tanganyika Broadcastinga Corporation katika medali ya kejeli na vichekesho.

Tofauti na walivyokuwa wakiigiza katika Independent Television [Tunamuomba Mzee Mengi afanye juu chini kupata vijana wengine watundu kama kina Masanja badala yao badala ya kupoteza muda wake mahakamani] kina Masanja sasa watatumiwa na TBC kwa niaba ya kuendeleza sera na mikakati ya CCM kuhujumu demokrasia na kusambaratisha upinzani chipukizi unaoanza kuota meno ya mwanzo kabisa hapa nchini.

Wale wote wanaotaka kuona Tanzania ikiwa na vyama viwili vikubwa kama vile kulivyo Marekani anakokuhusudu sana Mtawala wetu wa sasa, yaani Democrats na Republic.

Kweutu sisi Republics ni CCM na bila shaka kama Chadema na CUF tu [achilia wapuuzi wengine wanaoutumiwa na CCM wanaojiita wapinzani] basi Democrats watapatikana. [Tunawaomba wazee Lipumba, Sefu, Makani na Mtei wafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha CUF na CHADEMA wanaungana ikiwezekana mwishoni mwa mwaka huu ili kuhimili hujuma na janja ya CCM kupaka matope na kuwatumia wanaotumiwa katika nchi hii katika kueneza uwongo unaoharibia vyama vya upinzani kwa kuwatumia mamluki wa upinzani wakiwemo wachungaji, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na polisi ambao hawajui kwamba wanastahili kuwajibika kwa wananchi na sio kwa CHAMA FULANI!

Ninaamini Watanzaznia wote wanaokereketwa na mumo sawa na mfumo wa chama kimoja na wanaotaka kuona nchi hii inakuwa ya kidemokrasia halisi wataponda kipindi hicho na vipindi vingine vyote vya TANZANIA BLA BLAH CORPORATION na sio hivyo tu na kutaka maelezo kwanini kodi yao inatumika vibaya kuhudumu maendeleo ya demokrasia nchini!!!
 
Mzee ungekuwa muwazi zaidi kina masanja wanatumiwaje kwa niaba ya sisi ambao hatujaona hicho kipindi cha TBC.
 
Mzee ungekuwa muwazi zaidi kina masanja wanatumiwaje kwa niaba ya sisi ambao hatujaona hicho kipindi cha TBC.


Mzee Mndundu,

You don't need to ask any question... the post itself is "UPUUZI" na ni chombo kwa sasa kinachoheshimika sana...

Sio kila watu wanafikiri kijima... TBC ya sasa inafikiri vizuri zaidi hata ya hao private TV stations.

Angalia mpangilio wa taarifa zao you will know that!
 
Iga,labda kuna kitu unajua lakini unashindwa kukiweka sawa humu.Kwa sababu leo ndio hicho kipindi chao kipo saa moja nadhani.
Hebu tueleze basi wanawatumia kivipi,kabla ya wengi humu kuona kweli hii post yako haijakaa vizuri
 
Back
Top Bottom