TBC Kurusha Uchaguzi nchi nzima

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
na Mwandishi Wetu


amka2.gif

SHIRIKA la Utangazaji la Tanzania (TBC), linatarajia kurusha nchi nzima matangazo ya mwenendo wa zoezi la uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Tido Mhando, wakati akichangia mjadala juu ya wajibu wa vyombo vya habari katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ulioandaliwa na Shirika la Utangazaji la Ujerumani - Deutschevelle na kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, juzi.
Tido ambaye alikuwa ni mmoja wa wachangiaji wakuu katika mjadala huo, alisema TBC kupitia redio na televisheni itatuma wanahabari katika wilaya zote nchini kwa ajili ya kuripoti mwenendo wa zoezi la uchaguzi nchi nzima.
“Hatuna wanahabari wa kutosha, lakini tunaangalia uwezekano wa kuomba ushirikiano kutoka kwenye vyuo vinavyofundisha taaluma ya habari ili vitupatie kwa muda wanafunzi wake kwa ajili ya kufanikisha kazi hiyo siku ya uchaguzi,” alisema Tido. Katika hatua nyingine, washiriki mbalimbali wa mjadala huo, walisema vyombo vya habari nchini kumilikiwa na watu binafsi, hasa wafanyabiashara na wanasiasa, ni changamoto kubwa kwa vyombo hivyo kutimiza wajibu wake kwa haki katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwani upo uwezekano mkubwa kwa wamiliki hao kuvitumia kwa maslahi yao ya kisiasa badala ya maslahi ya umma. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya, alisema changamoto nyingine inayoikabili sekta ya habari nchini hasa katika kipindi hiki taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu, ni hulka ya vyombo vya habari kupenda kuripoti zaidi watu binafsi na matukio badala ya masuala ya msingi kama sera na ilani za vyama.

Hoja zangu:
Naungana na hoja ya Ananilea kwamba TBC ni lazima waripoti kwa fursa sawa za kunadi sera na ilani za vyama.Lakini pili wagombea wote wa chama cha mapinduzi na upinzani wapewe nafasi sawa bila kubagua uwezo wao kifedha. Hali kadhalika bila kujali umaarufu wa mgombea.
 
ndio maana watu hawachangii kwani tbc haina tofauti na redio uhuru kwani chombo cha ccm cha kukampenia...............tusubiri kama hatuamini haya...........nategemea kuona uozo wa tido mhando katika kupendelea wagombea wa ccm kwani nae ni kada mzuri
 
Hizo zote ni kodi zetu hivyo kurusha uchaguzi ni nzuri mashirika yote duniani ya serikali huwa yanafanya hivyo, VOA, BBC na nk huwa yanafanya hivyo
 
ndio maana watu hawachangii kwani tbc haina tofauti na redio uhuru kwani chombo cha ccm cha kukampenia...............tusubiri kama hatuamini haya...........nategemea kuona uozo wa tido mhando katika kupendelea wagombea wa ccm kwani nae ni kada mzuri

inaelekea hii inatakuwa mbeleko ya kumbebea mtoto fulani.
 
Hata Kampeni kwa kila Chama nazo warushwe bila ya kutoa pesa na pia kama kweli kodi zetu zinaweza kutumika, Hivyo kurusha matangazo ni jambo la msingi sana katika ulimwengu huu wa leo
 
Back
Top Bottom