TBC inamhitaji Dk. Rioba?

IslamTZ

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
309
182
Dk. Rioba angesoma hii ingemsaidia.

HUZUNI ndio ilikuwa hisia zangu za kwanza baada ya kusikia wiki illiyopita kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, John Magufuli amemteua Dk. Ayub Rioba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).

Huzuni yangu inatokana na ukweli kuwa Dk. Rioba alikuwa bosi wangu katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CKD) alipokuwa akihudumu kama Makamu Mkuu wa Shule hiyo.

Kama kumbukumbu yangu iko sahihi ni takriban mwaka mmoja tu tangu Dk. Rioba ateuliwe kushika wadhifa huo na tulishaanza kumzoea na kumuelewa.

Katika muda huo mfupi, tumemjua Dk. Rioba kama kiongozi anayetaka mabadiliko chanya na siku zote amekuwa chachu ya hamasa ya mabadiliko kwa sisi aliotuongoza.

Alituhimiza na kutusisitizia mara kwa mara kufanya kazi kwa bidii na kwa kufuata kanuni na maadili ya kazi ikiwemo kuhudhuria vipindi bila kukosa, kufundisha kwa weledi, kuandika makala za kitaaluma, kutafuta miradi na kadhalika.

Dk. Rioba aliongoza kwa mfano na ndio waliohuzunika kwa kuondoka kwake sio tu walimu wenzake bali pia wanafunzi wengi ambao wamemsifia kuwa ni mwalimu mzuri.

Mwanafunzi mmoja aliyekuwa akijaribu kuelezea uzuri wa Dk. Rioba kama mwalimu alisema: “Mwalimu Rioba amekuwa akitufundisha kama waandishi walio chumba cha habari na sio wanafunzi darasani, na hiyo ndio tofauti ya Dk. Rioba na walimu wengine.”

Fursa adhimu kwake
Nikiweka pembeni ubinafsi wangu, kwa Dk. Rioba kuonekana na Rais na hatimaye kuteuliwa kuongoza TBC ni fursa adhimu kwa maendeleo yake binafsi.

Kwa sababu hiyo basi, nitakuwa ni binadamu mwenye roho mbaya sana nikiangalia uteuzi wake kwa mtazamo wa SJMC kupoteza tu, bila kuzingatia kuwa hiyo ni fursa kwa Dk. Rioba ya kung’arisha wasifu wake wa kitaaluma na kiutendaji.

Dk. Rioba amekaa muda mrefu SJMC na kuhamia TBC kama Mkurugenzi Mkuu kutamsaidia kumjenga zaidi ili aweze kupambana na changamoto mpya katika tasnia ya habari, nje ya taaluma.

Licha ya kuondoka katika kipindi ambacho SJMC inamuhitaji zaidi, ukweli ni kwamba ameshatoa mchango mkubwa na wa kutosha katika nyanja ya taaluma. Kwa hiyo mwisho wa siku napenda kusema hongera Dk. Rioba kwa kuteuliwa Mkurugenzi wa TBC.

TBC inamhitaji Rioba
SJMC ilikuwa bado inamhtaji sana Dk. Rioba, lakini huenda TBC inamhitaji zaidi.
Sio siri kuwa vyombo vya habari vya TBC vinakabiliwa na changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kutoaminika mbele ya umma.
Hivyo basi, TBC inapaswa kujenga heshima yake mbele ya wananchi wengi kama shirika la taifa. Yapo mambo ya aibu ambayo yamewahi kufanywa na TBC na hivyo kupelekea watu kukichukia chombo hicho.

Wakati wa kampeni, kulisambaa video iliyoonesha mtangazaji wa TBC akisoma magazeti ambapo kwa makusudi alikwepa kusoma baadhi ya habari zilizohusu wapinzani. Lile lilikuwa ni tukio la wazi sana na ambalo sikusikia kuwa lilikemewa na viongozi wa shirika hilo au serikali. Yapo matukio mengine mengi.

Ni mambo kama hayo ndiyo yanayofanya watu waiweke TBC katika kundi moja na vyombo vya habari vya Chama cha Mapinduzi (CCM) kama gazeti na redio Uhuru.

Hii siyo TBC ninayotarajia kuiona chini ya uongozi wa Dk. Rioba ambaye amejijengea heshima miongoni mwa wanataaluma, watendaji, wanaharakati na hata mbele ya hadhira ya vyombo vya habari vya ndani na nje kama mchambuzi wa mambo, mwanahabari mahiri na mweledi anayejua anachokifanya.

Chini ya Dk. Rioba, tunategemea kuiona TBC mpya isiyopendelea upande mmoja, inayotoa fursa kwa usawa baina ya watawala na wapinzani na vile vile kumulika mambo muhimu yanayohusu makundi mengine ya kijamii, hususan yale ya watu wachache.

Wananchi pia wanategemea maboresho ya kiufundi ya vyombo vya TBC ikiwemo vifaa na rasilimali watu kimafunzo, maslahi na kupandisha morali ya kazi.

Hayo sio matumaini yangu tu bali ni matumaini ya wengi wanaomjua Dk. Rioba. Wengi tumejenga matumaini haya licha ya kuelewa uzito wa jukumu la kuongoza TBC.

Katika kuongoza TBC, mambo mawili yanaweza kutokea. Aidha muhusika atiwe msukosuko na kutakiwa kutii matakwa ya wanasiasa waliomteua na kuishia kufanya kazi za uenezi wa chama. Au mteule akomae na kuliekeza shirika katika muelekeo sahihi unaopaswa kwa shirika linsalotambulika kama la utangazaji la taifa – lakini kwa kufanya hivyo akijua kuwa anahatarisha ajira yake.

Sioni uwezekano wa Dk. Rioba kufanya kazi za uenezi wa chama katika shirika ambalo anajua fika kuwa ni la utangazaji la taifa. Dk. Rioba amejijengea heshima kubwa sana kukubali hilo litokee na heshima yake ishuke hivi hivi. Ndio maana kama ningeombwa nibashiri ningesema naona siku bora za TBC ziko usoni.

Kwa hiyo nataka kuamini kuwa kuondoka kwa Dk. Ayub Rioba SJMC ni kwa maslahi ya taifa – kutokana na matunda yatakayopatikana kutokana na uongozi wake.

Pia, mara nyingi huwezi kujua uwezo halisi wa watu mpka uwape fursa ya kuvaa viatu vikubwa kitaaluma, kiweledi, kiuongozi kama vya Dk. Rioba. Kuondoka kwa Rioba ni changamoto ya wanataaluma wachanga kuziba nafasi hiyo na kuonesha vipawa vilivyojificha walivyobarikiwa.

Faraja nyingine kubwa kwa SJMC ni kuwa Dk. Rioba bado anaweza kurudi SJMC kama mwalimu wa nje na hivyo kuwapa nafasi wanafunzi ya kuendelea kufaidika na utaalamu wake.

Faraja kubwa zaidi katika hilo ni kuwa Dk. Rioba atakuwa akija chuo kufundisha akiwa na mifano hai na mizuri zaidi ya kusaidia wanafunzi kuelewa vizuri zaidi masomo anayofundisha hususan lile alipendalo sana la maadili ya uandishi wa habar

Chanzo: Raia Mwema
 
Back
Top Bottom